loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bil 3/- zatumika kujenga jengo la Mkurugenzi

SERIKALI ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk John Magufuli imetoa zaidi ya shilingi bilioni tatu kutekeleza mradi wa ujenzi wa jengo la ofi si ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.

Akitoa taarifa ya mradi huo kwa Kamati ya Siasa ya CCM ya Mkoa wa Ruvuma,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Kassim Mpenda alisema mradi ulianza kutekelezwa mwaka 2017 umelenga kutatua changamoto ya uhaba wa ofisi unaowakabili watumishi wa Halmashauri hiyo na wananchi.

“Mradi huu hadi sasa umepokea zaidi ya Sh bilioni tatu kutoka serikali kuu, kiasi cha zaidi ya Sh bilioni 1.9 kimekwishatumika katika jengo hili,”alisema Mpenda.

Hata hivyo, alielezwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme alimsimamisha kazi Mkandarasi TBA ya ujenzi na Juni 6 mwaka huu, baada ya mkandarasi huyo kupata changamoto ya kufungiwa akaunti zake zote na kushindwa kuendelea na kazi, hali iliyosababisha halmashauri kutumia force akaunti kukamilisha mradi huo.

Alisema mradi wa jengo hilo hivi sasa upo katika hatua za umaliziaji ukiwa umefikia asilimia 82 kwa ujumla wake na kwamba mradi unatarajia kukamilika Agosti 30 mwaka huu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho ameushauri uongozi wa halmashauri hiyo kufanya kazi mchana na usiku ili kukamilisha kazi kwa sababu mradi huo umechelewa kukamilika na wananchi wanausubiri kwa hamu.

“Sisi Chama Cha Mapinduzi tunataka wakati wa kampeni Agosti mwaka huu tuwaambie wananchi wa Madaba kuwa tuliahidi, tumetekeleza kujenga jengo la Halmashauri, mkichelewa mtatuangusha’’,alisema.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Madaba

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi