loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jafo akerwa na ukusanyaji mapato Same

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo (pichani), amesema haridhishwi na ukusanyaji wa mapato katika halmashauri ya wilaya ya Same, ambao unashuka mwaka hadi mwaka.

Alisema mwaka juzi wilaya hiyo ilikusanya mapato kwa asilimia 87, mwaka jana asilimia 70 na mwaka uliomalizika ni asilimia 60 jambo ambalo halikubaliki.

“Nitoe wito kwa halmashauri yenu na nyingine nchini kubadilika na kukusanya mapato kikamilifu..... wizara yangu ilisemwa sana kuwa na mawaziri mizigo, hilo nimelifuta, ukiwa mzembe utaondoka wewe, hatuna utani na hilo,” alisema.

Aidha Waziri Jafo alisema serikali itaendelea kuwaondoa kazini, baadhi ya watendaji ambao wanakwamisha shughuli za maendeleo kwa makusudi na sanjari na wale vyanzo vya migogoro.

Alitoa mfano wa migogoro mikubwa na ya mara kwa mara baina ya mkuu wa wilaya hiyo, Rosemary Senyamule na aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Anna- Claire Shija ambaye kwa sasa hayupo.

“Hapa mlikuwa na migogoro ya hovyo hovyo, kila mmoja ameota pembe, hamuambiliki, nashukuru sasa kazi zitafanyika,mmepata mkurugenzi mpya,” alisema.

Alitaka watendaji wote kwa ujumla kutekeleza wajibu wao ikiwamo kukagua shughuli za maendeleo na kusimamia utekelezaji wa miradi kulingana na thamani ya fedha zinazotengwa na serikali.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo, Senyamule alisema wilaya imejitahidi kupunguza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa kwa kujenga zaidi ya vyumba 200 kati ya mahitaji ya vyumba 735.

Alisema kati ya vyumba vilivyojengwa, 192 vimejengwa kwa nguvu za wananchi, vyumba 41 vimejengwa na serikali na vyumba 32 vimejengwa na wadau wa maendeleo.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Nakajumo James, Same

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi