loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wajasiriamali mili 1.6 wapata vitambulisho

J UMLA ya vitambul- isho maalumu milioni 1.59 vya wafanyabiashara wadogo maarufu wamachinga ambao mtaji wao hauzidi Sh milioni nne vilivyotolewa kwa kundi hilo Desemba mwaka 2018 hadi Juni mwaka 2020 na viliingizia serikali Sh bilioni 31.86.

Fedha hizo zilitokana na mauzo ya vitambulisho hivyo kwa kundi hilo ambalo Rais John Magufuli ndiye aliyebuni wazo hilo na kutoa vitambulisho hivyo vilivyouzwa kwa Sh 20,000 kwa kila kimoja, ili wafanyabi- ashara hao wadogo wafanye kazi zao hizo kwa uhuru na kutambuliwa bila kubughudhiwa.

Kaimu Mkurgenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA ), Richard Kayombo alisema hayo wakati akizungumza na HabariLEO katika ma- onesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yanayomalizika leo katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumzia mapato hayo, Kayombo alisema wazo la Rais kwa kundi hilo ambalo halikuwa lim- erasimiwa na kutambulika, limekuwa lulu kwa kuwa kiasi hicho cha fedha kis- ingeweza kukusanywa kwa njia yoyote kutoka kundi hilo na kwamba hilo ni somo zuri litakalotumika kuonesha jinsi ushiriki hata wa mtu wa kipato cha chini ana- vyoweza kuchangia mapato ya serikali.

Vitambulisho hivyo vilianza kutolewa Desemba mwaka 2018 ambapo Rais Magufuli kwa kuanza alitoa vitambulisho maalumu 670,000 kwa wakuu wa mikoa yote ya Tanzania, ili kuwagawia wajasiria- mali wadogo kwenye mikoa yao ambao kipato chao ni chini ya Sh milioni nne kwa mwaka.

Kayombo alisema ka- tika utoaji wa vitambulisho hivyo, vyote viliisha na kuongezewa vingine ambapo hadi kufika Juni 2020 jumla ya vitambulisho 1,598,466 viliuzwa kwa wajasiriamali kwa bei ya kwa Sh 20,000 kila kimoja na kuipatia serikali jumla ya Sh 31,865,923,850.

“Mtakumbuka Rais Magufuli Desemba 2018 alizindua utoaji vitambulisho alivyobuni kwa wafanyabi- ashara wadogo nchi nzima na kutaka wasisumbuliwe na mtu yeyote wakati wa kufanya shughuli zao, Katika wazo hilo zaidi ya Sh bilioni 31.8 zilipatikana, fedha ambazo zisingeweza kukusanywa kutoka kundi hilo kwani ni kundi ambalo lilikuwa halijarasi- mishwa wala kutambulika kama linaweza kuchangia kiasi hata kidogo cha pato la serikali,”alisema Kayombo.

Kayombo alisema vitambulisho hivyo vimeleta tija kwani baadhi ya wajasiriamali hao wametoka kwenye kundi hilo la wamachinga wa kipato cha chini na kuingia wa kipato cha kati ambao wamepata sifa za kuchangia kodi ya serikali, hivyo kutoa nafasi kwa wengine kutumia vitambulisho hivyo.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Na Ikunda Erick

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi