loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzania kinara makadirio ukuaji uchumi Mashariki mwa Afrika

TANZANIA ni ya kwanza kati ya nchi 13 za Ukanda wa Mashariki mwa Afri- ka kwa kuwa na makadi- rio ya juu zaidi ya ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) la asilimia 5.2 pamoja na tishio la kiuchumi linalotokana na ugonjwa wa Homa kali ya mapafu inayosababishwa virusi vya corona.

Ripoti mpya ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imebainisha hayo na kueleza kuwa pamoja na tishio la kuporomoka kwa uchumi kwa nchi za ukanda huo kutokana na athari za ugonjwa huo, Tanzania inaongoza kwa ukuaji chanya wa GDP.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyowekwa na Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Has- san Abbasi katika ukurasa wake wa twitter, Tanzania ina makadirio ya juu zaidi ya ukuaji wa GDP kati ya nchi 13 za ukanda huo ka- tika kipindi cha Covid-19.

Katika ripoti hiyo kwa nchi 13 za mashariki mwa Afrika, Tanzania inaongoza kundi la ukuaji chanya wa GDP kwa asilimia 5.2 ikifuatiwa na Rwanda yenye asilimia 4.2. Ethiopia asilimia 3.1, Uganda yenye asilimia 2.5 na Kenya yenye asilimia 1.4.

Nchi nyingine zilizo katika ukuaji chanya na asilimia zake kwenye mabano katika ripoti hiyo ya mwaka huu (2020) iliyotolewa na AfDB kupitia taasisi yake inayofuatilia mwenendo wa uchumi Afrika (African Economic Outlook 2020), ni Djibouti (1.0) na Eritrea (0.3).

Kwa upande wa nchi zilizoathirika kwa kiwango kikubwa cha hasi kutokana na Covid-19 inayoongoza ni Shelisheli kwa asilimia -10.5, na Sudan (-7.2). Sudan kwa mujibu wa ripoti ya GDP za nchi hizo kabla ya ugonjwa huo ilikuwa nchi pekee katika kundi la ukuaji hasi kwa asilimia -1.6 katika ukanda huo wa mashariki mwa Afrika.

Nchi nyingine katika kundi la ukuaji hasi kipindi cha ugonjwa huo ikimaani- sha zilizoathiriwa na Covid-19 kwa kiasi kikubwa ni Burundi (-5.2), Somalia (-3.3), Comoro (-1.2) na Sudan Kusini (-0.4).

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Na Gloria Tesha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi