loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shehe Ponda akamatwa na Polisi kwa uchochezi

J ESHI la Polisi jijini Dar es Salaam linamshikilia Katibu Mkuu wa Jumui- ya na Taasisi za Kiislaamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alithibitisha kushikiliwa kwa kiongozi huyo akituhumiwa kufanya uchochezi kupitia waraka unaohusu Uchaguzi Mkuu alioutoa hivi karibuni.

“Ni kweli tunaye, amekamatwa kutokana na uchochezi katika hicho alichokiita waraka,” alieleza Mambosasa alipozungumza na HabariLEO jana.

Kamanda huyo alieleza kuwa, kiongozi huyo binafsi alikubali kwamba waraka walioutoa ni wake na taasisi yake, lakini viongozi wote wa taasisi hiyo wameukana kupitia vituo mbalimbali vya radio na televisheni.

Alisema kwa sasa jeshi hilo linaendelea na upelelezi kuhusu tuhuma hizo na ukishaka- milika litawasilisha jalada la mashtaka kwa Mwanasheria Mkuu na ndipo Shehe Ponda atakapopandishwa kizimbani kujibu mashtaka yake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa kwenye mitan- dao ya kijamii kiongozi huyo wa dini alikamatwa akiwa anatoka Msikitini kuswali swala ya Alasiri saa 11:00 jioni maeneo ya Ilala. Julai 9, mwaka huu, Shehe Ponda alipozungumza na waandishi wa habari alitoa wito wa kufanyika uchaguzi huru na wa haki Oktoba, mwaka huu.

Alisema katika waraka uliotolewa na taasisi hiyo umeorodhesha baadhi ya sifa hizo kuwa ni mgombea awe mkweli na mwenye utu, awe mwenye kuheshimu kiapo, awe mwenye sifa ya kupiga vita ubaguzi wa aina zote na awe mwenye maarifa ya kutosha ya kuongoza watu na serikali.

Sifa zingine zilizoainishwa kwenye waraka huo wa Ju- muiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania ni mgombea awe mwenye kuheshimu uhuru na mawazo ya watu wengine, mbali na kuzijua na kuziheshimu haki za binadamu. Kadhalika taasisi hiyo ya Waislamu wa Tanzania imetaka wananchi wasiwachague watu madikteta na wadhalilishaji katika uchaguzi huo wa Oktoba.

Pia alisema serikali imeshindwa kushughulikia ugonjwa wa Covid-19 na hakuna tume huru ya uchaguzi.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Na Halima Mlacha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi