loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri Kigwangallah apata mpinzani Nzega

WATIA nia wapya kugombea ubunge Majimbo ya Nzega Vijijini, Manyoni Mashariki na Ulyankulu wamejitokeza licha ya wabunge waliomaliza muda kuonesha nia kutetea nafasi.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kingwangala ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini (CCM) aliyemaliza muda wake, amepata mpinzani jimboni humo baada ya John Doto (CCM) kutangaza nia kuwania jimbo hilo.

Akizungumza kwa simu kutoka Dodoma jana, Doto, mwandishi wa habari na mjasiriamali, alisema uamuzi wake umezingatia msingi wa katiba na haki ya mtu kuchagua na kuchaguliwa.

Alisema alisukumwa na matatizo sugu yaliyomo jim- boni humo ikiwemo uma- sikini wa kipato, ubovu wa mindombinu ya barabara, elimu duni, maji na kilimo kilichokosa mwelekeo ikizingatiwa wananchi ni wakulima asilimia 80.

Mwingine aliyetangaza nia ya kuwania ubunge Jimbo la Manyoni Mashariki ni Eric Kuhoga (CCM), Mratibu wa asasi ya kiraia (NGO) ya Spiritual Life in Christ (SLIC) ya mjini Tabora. Jimbo hilo lilikuwa lilikuwa chini ya Mbunge aliyemaliza muda wake, Daniel Mtuka.

Kuhoga alisema pia anamheshimu Mtuka na uamuazi wake usichukuliwe kama ni utovu wa nidhamu kwani kuomba uongozi na uwakilishi wa wananchi ni haki ya kila raia wa nchi hii. Katika Jimbo la Ulyankulu ambalo Mbunge wake alikuwa John Kadutu ambaye amemaliza atalitetea akikabiliana na upinzani ku- toka kwa Selemani Onesmo (CCM) mfanyabiashara wa madini Kata ya Silambo Wilaya ya Kaliua.

Selemani alisema jambo kubwa ni kujenga uhusiano na wananchi ku- weka mazingira mazuri ya kuwashirikisha wananchi na kuwa na imani ya uchangiaji michakato ya maendeleo katika sekta zote siyo kuan- galia maslahi binafsi.

Aidha, katika udiwani kata ya Usinge, Kaliua Titus Kavula (CCM) ametangaza kuwania udiwani wa kata hiyo iliyochukuwa na Cor- nery Malabe wa Chama cha ACT- Wazalendo.

Kata nyingine ni Kalola Wilayani Uyui ambapo Sauji Daud (CCM) ametangaza nia kuwania udiwani iliyokuwa ikiongozwa na Abdalah Koni na Haruna Kulwa (CCM) ametangaza kuwania Kata ya Itetemia iliyokuwa Chadema.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Na Lucas Raphael, Tabora

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi