loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Daladala zitakazosimamisha abiria kukiona

TRAFIKI Kanda Maalum Dar es Salaam imese- ma haitasita kufuta leseni, kuandika faini na kukamata gari kwa dereva yeyote anayekiuka agizo la kutosimamisha abiria lililowekwa baada ya kutokea mlipuko wa virusi vya corona.

Mkuu wa Trafiki Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Marson Mwakyoma alisema hayo alipozungumza na HabarLeo kuhusu katazo hilo la kusimamisha abiria lililotolewa ili kulinda afya ya abiria wawapo kwenye magari.

Kuhusiana na agizo hilo, Mwakyoma aliwataka wamiliki kuwasisitiza madereva wanaoendesha magari yao kufuata maelekezo hayo kwani kinyume chake wataingia hasara ambayo itatokana na kukamatwa kwa magari hayo.

“Tutakamata madereva wakaidi watakaporudia kosa mara ya pili na ya tatu tutachunguza walikosoma, mikataba yao na leseni zao ni daraja gani kisha tutawa- fungia,” alisema.

Alisema suala la kusimama abiria kwenye mabasi ya abiria lilitolewa amri na mamlaka husika na hadi sasa agizo hilo halijatenguliwa.

Alishauri wananchi waliokaa kwenye viti kutoa taarifa wanapoona gari linasimamisha abiria ama linabeba zaidi na kuwaambia wachuchumae kwani hiyo haikubaliki.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Na Lucy Ngowi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi