loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzania yaweka rekodi sekta ya madini

SERIKALI ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk John Magufuli, imevunja rekodi katika mapato kwenye sekta ya madini, kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanywa na serikali hiyo kwenye sekta ya madini.

Mageuzi aliyoyafanya Rais Magufuli katika miaka yake mitano ya kuendelea yanahitaji kufanyiwa dhukuru (tafakuri) sana. Hayo yalibainishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi wakati akizungumza kwenye kipindi cha Dhukuru ya Msemaji, kinachorushwa na Televisheni ya Maelezo.

Dk Abbasi alitoa mfano kuwa mwaka huu wa fedha, serikali ilipanga kukusanya mapato katika sekta ya madini yanayofikia kiasi cha Sh bilioni 470, lakini hadi Mei 31 mwaka huu, mwezi mmoja kabla ya mwaka wa fedha kwisha, ilivuka lengo kwa kukusanya Sh bilioni 479.45.

“Moja ya maeneo ya mageuzi ya Dk Magufuli ni kwenye sekta ya madini. Alipoahidi mabadiliko ya kweli kwenye kampeni, alizungumzia mageuzi kuhakikisha si tu tunakuwa na madini na kubaki na mashimo, bali yanakuwa na manufaa kwa watanzania,” alisema Dk Abbasi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Hata hivyo, alisema baadaye baadhi ya watu walianza kutoa vitisho, ikiwemo kudai kuwa hatua zilizochukuliwa kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko hayo, zinaweza kuipeleka nchi pabaya jambo ambalo halikutokea.

“Baadaye tukaanza kutishana, leo kwa maana ya kufanya dhukuru (Tafakuri) leo tunapozungumzia sekta ya madini hakuna kupelekwa miga wala mwiba, mageuzi yamefanyika, mikataba karibia kampuni zote kubwa imeanza kufanyiwa kazi, imeanza kupitiwa ili kuhakikisha nchi inafaidika,” alisisitiza.

Alisema katika eneo ambalo serikali imepata mafanikio makubwa ni kukubaliana na Kampuni ya Barrick na kwa pamoja wakaunda Kampuni ya pamoja ya Twiga Minerals Corporation Limited.

“Kwa kwa mara ya kwanza tunamiliki kampuni, sisi na mwenye mtaji na sisi ndio wenye madini” alisema.

Dk Abbasi alisema kampuni hiyo, imeanza kufanya kazi, ambapo pia serikali imelipwa fedha kiasi cha Sh bilioni 250 kama sehemu ya mabilioni mengine yanayokuja.

Hata hivyo, alisema katika mfumo wa umiliki wa Twiga Minerals pamoja na kumiliki kampuni hiyo, mapato ya jumla kwenye kikotoo Tanzania kama nchi, nayo itafaidika kuelekea ama kuwa sawa asilimia 50 kwa 50 na wengine.

“Tutapata kodi nyingi, tutalipwa hisa zetu kwa ujumla si tu kumiliki hisa zile 16 kama hisa za Twiga Minerals, lakini manufaa ya kiuchumi yatakwenda kwenye 50 kwa 50 na kuna wakati sisi tutakuwa tunazidi kidogo,” alifafanua.

Alisema sekta ya madini jinsi ilivyokuwa na sasa, imekuwa na mageuzi makubwa, ikiwemo Rais Magufuli kuzuia makaboni, kuanzisha masoko ya madini na sasa kila mkoa makusanyo na mapato.

HISA milioni 15 zenye thamani ya shilingi ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi