loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mkapa alitamani kufa kabla ya miaka 86

RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa (81) akiwa kwenye makazi yake mwaka jana, kijiji cha Mkuzi wilayani Lushoto, Tanga alisema anatamani kufa kabla ya miaka 86.

Hayo yalibainishwa wakati mwandishi wa habari hii alipokuwa akizungumza na jirani wa Mkapa kijijini hapo, Caroline Mganga (62) kuhusu mambo mbalimbali yanahusu maisha ya kiongozi huyo kwenye kijiji hicho.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano hayo:

Mwandishi: Kabla ya kufikwa na umauti, je ni lini mara ya mwisho alifika Lushoto, na alizungumza neno gani?

Caroline:Unajua marehemu alikuwa na kawaida kila mwisho wa mwaka anakuja Lushoto, alikuwa anajumuika na wanakijiji wenzake tunasheherekea kumaliza mwaka na kukaribisha mwaka mpya.

Kwa mara ya mwisho alikuja mwezi Desemba mwaka 2019, alikuja kushukuru kutimiza miaka 80. Baada ya kutoka kanisani, maana tunasali wote kanisa moja nyumbani alisema kuwa nashukuru nimepita miaka 70 na sasa 80 namuomba Mungu nisifike miaka 86…alinishtua nikamuuliza kwa nini je, una ahadi na Mungu? akanijibu kuwa katika sala zake, huwa anamuomba Mungu asife akiwa amechoka sana na asingependa kifo chake kiwe cha usumbufu.

Mwandishi: Kwa mara ya kwanza ulifahamiana vipi na Rais Mkapa?

Caroline: Nakumbuka kwa mara ya kwanza kufahamiana na Rais Mkapa ilikuwa ni mwaka 2001 wakati alipowatuma akina Hassan Ngwilizi aliyekuwa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) katika Serikali ya Awamu ya Tatu aliyokuwa anaiongoza.

Ngwilizi alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Mlalo na Fanueli Kuzilwa aliyekuwa Mnikulu wa Ikulu na Mama Caroline George mmiliki wa Hoteli ya Uswisi iliyopo hapa Lushoto, ndipo katika kutafuta eneo wakapata hapa Mkuzi karibu na nyumbani kwangu, sasa mimi nikawa nafahamiana na mtu aliyekuwa mmliki wa eneo hilo.

Nakumbuka kipindi kile baaada ya kuja kuulizia eneo hilo ambapo ni karibu na nyumba ya marehemu Ngwilizi wakaniachia mimi jukumu la kumtafuta mwenyewe ambaye Mzee Chamsama ambaye kwa sasa ni marehemu.

Wakati huo lilikuwa chini ya uangalizi wa mwanawe Clara Chamsama na hadi kufikia mwaka 2003 ndipo taratibu za kuuziana zikafanyika na mimi nikawa ni miongoni mwa waliohakikisha mzee Mkapa amekabidhiwa vielelezo vyote.

Kuanzia kipindi hicho hadi mwaka 2005 alikuwa anafanya ukarabati hadi kukamilika na mwanzoni mwa mwaka 2006 Rais Mkapa alikuja kufungua rasmi makazi yake mapya baada ya kustaafu urais.

Alifanya sherehe kubwa, alialika wanafunzi wa shule za jirani zinazozunguka pamoja na wanakijiji.

Mwandishi:Je, baada ya hapo ukaribu wenu uliisha?

Caroline:Kwa kweli baada ya hapo ujirani wetu ndio ukawa wa karibu sana, kila alipokuwa akiondoka aliniachia majukumu ya kuwa muangalizi wa nyumba yake na walinzi na wakati mwingine hadi fedha za kuwalipa watumishi alikuwa ananitumia mimi.

Mwandishi:Katika muda alioishi hapa Lushoto Mzee Mkapa hadi kukutwa na umauti ni jambo gani umejifunza kutoka kwake?

Caroline:Jambo kubwa nililojifunza kutoka kwake huyu alikuwa ni mtu mnyenyekevu kwa kila mtu bila kujali cheo chake kuwa alikuwa Rais, yaani yeye kila alipokuja Lushoto kila mwanakijiji aliyemuendea kumuelezea shida yake alimsikiliz na alikuwa hajikwezi.

Mwandishi:Ni jambo gani kubwa ambalo Mkapa katika uhai wa maisha yake ulimfurahisha?

Caroline:Jambo ambalo Mkapa nililomfurahisha ambapo kila akikaa alikuwa ananikumbuka ni jinsi nilivyopambana kuhakikisha anapata eneo la pili Lushoto japokuwa baadaye hakuweza kulinunua.

Mwandishi:Unasema kila alipokuwa akija Lushoto mtu wa kwanza kukuita ni wewe na mlikuwa kwenye chakula mnajumuika pamoja je, ni aina za vyakula gani alikuwa anapenda?.

Caroline:Vyakula nilivyokuwa nikimuona anapendelea akija Lushoto ni pamoja na ugali, wali, mboga za majani haswa mchemsho.

Mwandishi:Jambo gani kubwa alilokufanyia ambalo hutalisahau katika maisha yako?

Caroline:Mh! Mambo mengine ni siri ila amenifanyia makubwa kwa kweli namshukuru

Mwanaidi Bilali, mkazi wa kijiji cha Matandu, wilayani ...

foto
Mwandishi: Cheji Bakari, Lushoto

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi