loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kikwete: Rais Magufuli ana kazi kubwa kuelekea 2025

Kikwete: Rais Magufuli ana kazi kubwa kuelekea 2025

RAIS wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete amesema Rais Magufuli ana kazi kubwa ya kuhakikisha anasimamia misingi iliyoachwa na Hayati Benjamin Mkapa.

Kikwete alimeyasema hayo katika mazishi ya Mkapa kijijini Lupaso, Masasi mkoani Lindi.

"Mkapa wakati ameingia madarakani, aliipokea ikiwa na hali sio nzuri, lakini alisimamia, katika miaka mitano yake mitano ya mwisho alipandisha uchumi wa nchi na aliacha uchumi ukiwa umekuwa kwa asilimia Saba,"amesema Kikwete na kuongeza;

“Magufuli ana kazi kubwa ya kuhakikisha anatutoa katika asilimia saba na kutufikisha asilimia nane au 10 ifikapo 2025, kazi kubwa anayo.”

Misingi aliyoacha Mkapa maana yake wanaomfatia wanapaswa kuendelea kuidumisha, misingi hiyo pato la Mtanzania lifike dola 3,500.

Amesema, Mkapa amefanya kazi yake ameimaliza salama.

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi