loader
Watakiwa kuboresha maonesho Nanenane Nyanda Juu Kusini

Watakiwa kuboresha maonesho Nanenane Nyanda Juu Kusini

WADAU wa Maenesho ya Wakulima (Nanenane) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wametakiwa kuanza kufikiria namna ya kuyaboresha maonesho hayo ili yawe na mwonekano tofauti na ilivyozoeleka.

Uendeshaji wa maonesho hayo unaotegemea michango ya halmashauri umetajwa kupitwa na wakati, badala yake wadau wametakiwa kufikiria namna mpya ya kupata michango ya kuyaendesha.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesera, alitoa wito huo wakati akifungua kikao cha mwisho cha Maonesho ya Nanenane 2020, kilichofanyika jijini Mbeya juzi.

“Kuendelea kuzitegemea halmashauri kuendesha maonesho hayo ni mzigo mwingine kwa serikali na ipo siku inaweza kutokea uongozi wa nchi ukaamua vinginevyo iwapo mzigo huo utaendelea kuwapo,” alisema.

Kasesera alisema ni wakati sahihi kwa wadau kuanza kufikiria vyanzo vipya vya kuendesha maonesho hayo, ikiwamo kutafuta wafadhili hususan kampuni ambazo zimekuwa zikinufaika na uwapo wa maonesho hayo.

“Tunaweza tukaamua hata kampuni za vinywaji kuwa zitaruhusu zile tu zitakazokuwa zimetupa ufadhili ndiyo vinywaji vyao viuzwe humu uwanjani. Wasiotuchangia wateja wao watakunywa huko nje. Mtaona wenyewe kama hawajatufuata kutuchangia,” alisema.

Pia alisisitiza kuboreshwa kwa mazingira ya uwanja wa maonesho wa John Mwakangale, akisema unatakiwa uendane na sifa za mikoa inayoutumia ambayo ndiyo inayozalisha mazao mengi nchini.

 

 

foto
Mwandishi: Joachim Nyambo, Mbeya

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi