loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mkwasa sasa aitega Yanga

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa amesema kama klabu hiyo inamuhitaji kubaki kuwatumikia kwa ajili ya msimu ujao, basi ni kwa nafasi ya ukoch mkuu tu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkwasa alisema sababu ni kwa kuwa amegundua kuendelea kuwa kocha msaidizi anaweza kufanya kazi na makocha aliowazidi uwezo na matokeo yake akasababisha migogoro isiyokuwa na ulazima.

Licha ya kuwa mkataba wake unamalizika mwezi ujao, alisema mpaka sasa hafahamu mipango ya klabu hiyo dhidi yake akiweka msisitizo kuwa hayuko tayari tena kuwa kocha msaidizi.

“Kwa sasa siko tayari kuwa kocha msaidizi tena kwani wakati mwingine unakutana na makocha wasiokuwa na uwezo na pale unapomshauri jambo inaleta mgogoro,”alisema.

Mkwasa ambaye alikuwa kimya kwa mudahuku akishindwa kuonekana katika mechi mbili za mwisho za ligi dhidi ya Mtibwa Sugar na Lipuli aliamua kuvunja ukimya huo ikiwa ni siku chache zimepita tangu uongozi wa Yanga kutangaza kumtimua aliyekuwa Kocha Mkuu, Luc Eymael kutokana na kauli zake za kibaguzi.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania alisema sababu zilizokuwa zimekuweka kando ni yeye kuamua kujiweka pembeni baada ya kusikia kauli za Eymael kuwa hataki kufanya naye kazi.

“Wakati nilipoambiwa niwe kocha msaidizi, nilikubali kwa kuwa nilidhani nitajifunza mambo mengi kutoka kwa Eymael, baada ya kufanya naye kazi nikabaini ni kocha mwenye uwezo mdogo sana, nilijaribu kumshauri ilipofika wakati akaona kuwa hawezi kufanya kazi na mimi na kuwataka viongozi kuchagua kati ya mimi au yeye, kuepusha migogoro nikaomba nikae pembeni, ”alisema.

Alisema alijaribu kutimiza majukumu yake ya kumsaidia ili aweze kufanikiwa ikafika wakati akaona kama anamfundisha kazi na kumkataa.

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wametajwa katika tetesi ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi