loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Msumbiji kusafirisha gesi asilia Tanzania 2024

MSUMBIJI inajipanga kusafirisha gesi asilia kwenda Tanzania mwaka 2024 baada ya Kampuni ya Total ya Afrika Kusini kutoa mkopo wa dola bilioni 14.9 kwa ujenzi wa eneo la usindikaji wa gesi hiyo jimbo la Cabo Delgado  bonde la mto Ruvuma Kaskazini mwa nchi hiyo.

Makubaliano ya kuwekeana saini kwa ajili ya mkopo huo yalifanyika Julai 15, 2020.

Mradi wa gesi asilia eneo lenye utajiri wa gesi bonde la mto Ruvuma Kaskazini Mashariki mwa Tanzania unasubiri uamuzi wa mwisho wa  uwekezaji  baada ya serikali kutoa idhini yake.

Uamuzi wa Msumbiji kujenga eneo la mradi ulitolewa Juni 2019 na Agosti ujenzi ulianza.

Ofisa wa fedha wa Kampuni ya Total Afrika Kusin, Pierre Sbraire alisema mkopo huo ni moja ya mikopo mikubwa kutolewa Msumbiji ukijumuisha mawakala na mabenki 19 ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika ambayo ilitoa kiasi cha dola za Marekani milioni 400.

“Huu ni mkopo wa daraja la juu utakaoleta mapinduzi katika miradi mikubwa Afrika,” alisema Mshauri Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (Afdb), Souley Amadou wakati mazungumzo yake na wadau wa mradi huo pamoja na wawakilishi wa serikali ya Msumbiji.

Total Afrika Kusini inaongoza muungano wa mashirika katika mradi wa gesi eneo la  Afungi.

“Mradi utasaidia maendeleo ya gesi, umeme na kushika nafasi kubwa kuleta suluhisho la kuaminika kwa nishati kwa urahisi na gharama nafuu kwa nchi hiyo na maeneo jirani,” alisema Mkurugenzi wa fedha, sera na kanuni miradi ya nishati wa Benki ya AfDB,  Wale Shonibare.

foto
Mwandishi: MAPUTO, Msumbiji

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi