loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Zaidi ya wakazi 11,980 wafaidika mradi wa maji

ZAIDI ya wakazi 11,981 wa vijiji viwili vya Lilambo A na Lilambo B, kata ya Lilambo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, wameanza kunufaika na mtunda ya Serikali ya Awamu ya Tano baada ya kukamilika ujenzi wa mradi wa maji kwa gharama ya Sh 1,164,555.586.

Mradi huo, umejengwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira, Manispaa ya Songea (Souwasa) kwa kushirikiana na Wakala wa Maji Vijijini, Mkoa wa Ruvuma (Ruwasa).

Mradi wa maji Lilambo umetekelezwa chini ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) kupitia Programu ndogo ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP) unalenga kuwaondolea changamoto ya maji safi na salama wakazi wa vijiji hivyo viwili.

Hayo yalisemwa na Meneja Ufundi wa Souwasa, Jafar Yahaya mbele ya wajumbe wa Bodi ya Mamlaka hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Dk Anselem Tarimo iliyofanya ziara ya siku moja kukagua miradi ya maji inayojengwa na Souwasa katika wilaya tatu za mkoa wa Ruvuma.

Hata hivyo, kutokana na mabadiliko ya sheria ya usimamizi wa huduma za maji safi na usafi wa mazingira, mkataba wa mradi ulihamishwa kutoka wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini Ruwasa kwenda mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Songea-Souwasa na utekelezaji wake umefikia asilimia 98.

Alisemaujenzi wa mradi Lilambo unatekelezwa kwa awamu moja na kazi zilizopangwa kufanyika ni ujenzi wa chanzo cha kukusanyia maji, nyumba ya mashine na uzio wa mita 160 kuzunguka eneo hilo, usambazaji na ufungaji pampu, ujenzi wa visima na kusambaza bomba mita 4050 za kusafirishia maji umbali wa meta 10,790.

Jafari alitaja kazi nyingine ni kuchimba mitaro, ulazaji bomba za usafirishaji na usambazaji maji, ujenzi wa tenki la lita 150,000, uzio wa mita 80, vituo 18 vya kuchotea maji na chemba za maungio ya maji safi.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Souwasa), Patrick Kibasa alisema hadi sasa kazi zilizofanyika ni kujenga chanzo cha maji, visima, tenki la mita za ujazo 25, usambazaji na ufungaji wa pampu na transfoma ya umeme, kupima wingi wa maji katika chanzo na ujenzi wa kibanda cha mashine.

Kwa mujibu wa Kibasa, kazi nyingine zilizofanyika kulingana na mkataba wa mradi huo ni pamoja na ujenzi wa uzio mita 160, usambazaji na uchimbaji mitaro, kujenga vituo 18 vya kuchotea maji, chemba nne, ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji na ujenzi wa tenki la kutibu maji kutumia klorini.

Dk Tarimo aliipongeza Souwasa kwa kazi mzuri inayofanya katika kutekelezaji, kujenga miradi na kutoa huduma bora ya maji kwa wananchi.

Hata hivyo, aliwataka wanufaika wa mradi huo kuhakikisha wanatunza na kutumia maji hayo kuharakisha maendeleo yao kama ilivyokusudiwa na serikali kusogeza huduma ya  maji na kumtua mama ndoo kichwani.

KATIBU Tawala wa Wilaya ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Mbinga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi