loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watanzania tuviunge mkono viwanda vyetu

KAMA kuna mambo ambayo Watanzania tunapaswa kujivunia hivi sasa, ni uwepo wa bidhaa mbalimbali zinazoendelea kuzalishwa hapa nchini kupitia viwanda vyetu huku vingi ya viwanda hivyo vikimilikiwa na wazawa.

Uwepo wa viwanda mbalimbali vilivyoanzishwa na vinavyoendelea kuanzishwa hapa nchini, ni wazi kuwa Tanzania imeamka na inazidi kukua kiuchumi siku hadi siku kutokana na malengo mbalimbali ambayo imejiwekea kama Taifa kusonga mbele kimaendeleo.

Ikumbukwe kuwa kipindi cha nyuma, Tanzania ilikuwa moja ya mataifa yaliyokuwa yakitegemea zaidi bidhaa za aina mbalimbali zikiwemo za ujenzi zilizokuwa zikiingizwa kutoka mataifa mbalimbali ambazo baadhi hazikuwa na ubora ule unaotakiwa.

Angalau kwa sasa Watanzania wanaweza kusimama vifua mbele tena kwa moyo mkunjufu kabisa pindi wanapokwenda katika maduka kwa ajili ya kununua bidhaa mbalimbali wakiwa ana imani kuwa kwa sasa nyingi ya bidhaa zinazouzwa katika maduka hayo zimezalishwa nchini hivyo kuondoa ile hofu ya uwepo wa bidhaa bandia au zisizo na ubora.

Kutokana na kadhia hiyo ya uwepo wa bidhaa bandia kulisababisha uwepo wa malalamiko mengi zaidi; kutoka kwa watumiaji wa bidhaa hizo wakiwemo baadhi ya wafanyabiashara ingawa sehemu kubwa ya waliokuwa wakiingiza bidhaa hizo ni wao wenyewe.

Hakuna shaka kuwa hadi sasa bado wapo baadhi ya wafanyabiashara hao wanaoingiza bidhaa mbalimbali zisizo na ubora kutoka nje kwa akili ‘mbovu’ kuwa kufanya hivyo kunawasaidia kupata faida ya haraka suala ambalo binafsi naona ni ushamba uliopitiliza na zaidi wanapaswa kuchukuliwa hatua stahiki na mamlaka zinazohusika.

Jambo la msingi hapa Watanzania kwa umoja wetu tunapaswa kuwa pamoja na kushirikiana katika kuwaumbua wale wote wanaojiuhusisha na uingizaji au utengenezaji wa bidhaa zisizo na ubora kwa kuwa sote ni walaji wa bidhaa hizo.

Katika kukabiliana na hilo ni vyema pia kama Watanzania tukajifunga na kuacha kununua bidhaa kutoka nje na badala yake tujielekeze katika kununua bidhaa za ndani kwa kuwa nyingi zina ubora wa uhakika lakini pia tukitambua kwa kufanya hivyo tutakuwa tunakuza uchumi wa taifa letu.

Hivi karibuni Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo alisisitiza kuhusu suala la ununuzi wa bidhaa za ndani kwa kuziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha miradi yote ya ujenzi zikiwemo hospitali na shule zinatumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

MAOFISA Waandamizi wa Sekta ya Sheria wa Jumuiya ya Maendeleo ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi