loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali kutumia bilioni 331.7/- Uchaguzi Mkuu

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itatumia Sh bilioni 331.7 kwa ajili ya kuandaa na kuendesha Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu huku kitendo cha serikali kugharimia kwa asilimia 100 kikipongezwa na vyama vya siasa.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage alitoa taarifa hiyo kwenye kikao kati ya tume na vyama vya siasa kilichofanyika Dar es Salaam akisema jumla ya wapiga kura milioni 29.2 watapiga kura za madiwani, wawakilishi, wabunge na rais.

Ajenda kuu ya kikao ilikuwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 na mambo ya kuzingatiwa na vyama.

Alisema fedha hizo zimetolewa na Serikali kupitia Mfuko Mkuu wa Hazina kwa kuzingatia kifungu cha 122 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi na itagharimia shughuli zote za uchaguzi kwa asilimia 100.

Hatua hiyo ya serikali ya kugharimia uchaguzi peke yake imepongezwa na vyama vya Siasa. Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wakulima (AAFP), Rashidi Rai alisema:

“Kitendo cha kutumia fedha zetu kugharamia uchaguzi kinaonesha uhuru kamili tulionao lakini pia ni heshima kwa Taifa na Serikali yetu.” Sambamba na hilo, Jaji Kaijage alisema kwa mujibu wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, jumla ya wapiga kura milioni 29.2 watashiriki katika kupiga kura katika uchguzi mkuu ujao.

Alisema tume imekamilisha uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao ulifanyika mara mbili.

Katika awamu zote mbili za uboreshaji, wapiga kura wapya 7,326,552 waliandikishwa, wapiga kura 3,548,846 waliboresha taarifa zao 30,487 waliondolewa kutokana na kukosa sifa kwa mujibu wa sheria.

“Hivi sasa daftari lina jumla ya wapiga kura 29,188,347,”alieleza Jaji Kaijage.

Alisema kutokana na idadi hiyo ya wapiga kura, kutakuwa na vituo 80,155 vya kupigia kura na kila kituo kimoja kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500.

KATIBU Tawala wa Wilaya ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi