loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Samia: Vikao vya juu vitateua wagombea sahihi

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema vikao vya juu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), vitarekebisha na kupitisha wagombea sahihi wa chama hicho itakapobainika wajumbe katika ngazi ya kura za maoni waliteleza au kufanya machaguo yasiyo sahihi.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini hapa wakati akifungua Maonesho ya 27, ya Wakulima,wafugaji na wavuvi ambayo kitaifa yanafanyikia katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Alisema, “Niwatoe wasiwasi tunajua uchaguzi wa awali wa kura za maoni kupata wagombea ulishafanyika, msiogope pale wajumbe walipoteleza au kufanya chaguo lisilo sahihi tutarekebisha hayo kwenye vikao vya juu ili tuhakikishe mnapata viongozi bora kwa maslahi ya taifa na sio matumbo yao.” Kauli hiyo iliungwa mkono na wananchi waliokuwa wakisikiliza hotuba hkutokana na kushangilia.

Samia alisema ni lazima wapatikane viongozi bora watakaoweza kushirikiana na serikali kuleta maendeleo ya wananchi na siyo kujali maslahi binafsi.

“Niwatake tu uchaguzi mkuu chagueni wale watakaosimamia maendeleo yenu na watashirikiana na serikali msichague wenye kujali matumbo yao,hata kauli mbiu ya maonesho haya ni “Kwa Maendeleo bora ya uvuvi na kilimo, chagua viongozi bora’’.

Alisema viongozi wasio waadilifu ndio wanaochangia kuwapo kwa changamoto kutotatuliwa kero za wananchi hatua inayotokana na kutotimiza wajibu kwa kutaka rushwa na kujali maslahi binafsi kuliko kufanya kazi kwa ufanisi.

KATIBU Tawala wa Wilaya ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick, Bariadi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi