loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Samia azipa neno taasisi za fedha

TAASISI za fedha zimeagizwa kuongeza kiwango cha mikopo kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi kwani kwa sasa ni asilimia tisa tu ndio hutolewa licha ya sekta kuwa na mchango mkubwa kwa taifa.

Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan alitoa mwito huo jana wakati akifungua Maonesho ya 27 ya wakulima, wafugaji na wavuvi ambayo kitaifa yanafanyika wilayani Bariadi katika Mkoa wa Simiyu.

Pia Mama Samia alizindua miongozo miwili ya kitaifa ambayo ni, Muongozo wa Uongezaji wa Virutubisho na Mafunzo ya Lishe kwa wakulima na wa uongezaji virutubisho kibiolojia katika mazao ya chakula.

“Hadi sasa taasisi za fedha na benki zimetoa asilimia tisa tu ya fedha zote za mikopo kwenye sekta ya kilimo,kiasi hiki cha fedha ni kidogo wakati mchango wa kilimo ni mkubwa, ni lazima kiongezwe sasa, naziagiza benki ongezeni mikopo ya kilimo,” alisema.

Alisema Benki ya TIB imeidhinisha mkopo wa Sh bilioni 26 kwa ajili ya sekta ya kilimo wakati TPB imefungua dirisha maalumu kwa ajili ya mikopo kwa wakulima.

Alisema pia CRDB, NMB na Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) zimefanya hivyo. Wakati huo huo aliagiza watafiti wa mbegu bora kuhakikisha matokeo ya utafiti yanawafikia wakulima kupitia maofisa ugani iwe rahisi kuzitumia na kuja na matokeo bora.

Alisema utafiti mwingi wa masuala ya kilimo na mbegu uamefanyika na kuja na matokeo mazuri ya aina za mbegu zinazokabiliana na ukame na magonjwa lakini hazijawafikia wakulima wengi.

Agizo lingine alilotoa ni kuhakikisha eneo la umwajiliaji zinaongezeka kutoka hekta 475,000 za sasa na kuwa nyingi zaidi kwa sababu nchi ina eneo kubwa linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji lakini kinachotumika ni kidogo.

Akizungumzia mkakati wa kuboresha kilimo, Mama Samia alisema serikali imebuni mpango wa kuboresha wakulima na kujua mahitaji yao na kufanikiwa .

Alisema wameanza kusajili wakulima na hadi mwezi uliopita, wakulima 1,325,799 walikuwa wameshasajiliwa.

Wamesajiliwa kupitia mfuko maalumu wa kusajili wakulima na aina ya kilimo wanachofanya lengo likiwa ni kuwezesha serikali kuwa na idadi na kujua mahitaji yao kama vile zana za kilimo na pembejeo.

Mama Samia alisema serikali imekuwa ikiboresha sekta ya kilimo na kwamba mwaka 2019/20, idadi ya tani za mbolea iliyonunuliwa kwa ajili ya wakulima imeongezeka hadi kufika tani 604,978 wakati mwaka 2015/16 ilikuwa tani 302,000 Awali, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema wizara imejipanga kuhakikisha wakulima,wafugaji na wavuvi wanatekeleza kazi zao kitaalamu kuwa na tija.

Alisisitiza kwamba ni lazima mazao ya kilimo yaongezewe thamani kuwa na bei nzuri zaidi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema jambo kubwa la kuhakikisha sekta ya kilimo inaimarika ni kubadilisha mtazamo wa wakulima na wananchi kuhusu kilimo.

Aidha alipendekeza wizara ya kilimo ichague eneo maalumu litakalokuwa kituo cha maonesho ya wakulima kitaifa, kuliko ilivyo sasa ambapo kila baada ya muda siku hiyo huadhimishwa kwenye mkoa fulani.

MTOTO Juma Megejuwa (12) mkazi wa ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick, Bariadi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi