loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri aonya wamiliki vyombo vya usafiri

SERIKALI imeliagiza Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (Tasac) kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa vyombo vya usafi ri na kuchukua hatua dhidi ya wamiliki wanaokiuka sheria za usafi rishaji.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alitoa agizo hilo kwa niaba ya serikali kufuatia tukio la ajali ya kuzama Boti ya Abiria Mv Baba Philipo iliyotokea Ziwa Tanganyika katika kijiji cha Lufubu, kitongoji cha Kamakala, wilayani Uvinza mkoani Kigoma na kusababisha vifo vya watu 13.

Kamwele pia aliagiza Tasac kuchunguza chanzo mahsusi cha ajali hiyo na kubaini upungufu na makosa yaliyofanyika ili hatua kali za kisheria zichukuliwa kwa wote waliohusika.

“Nimepokea kwa mshtuko na masikito makubwa taarifa ya ajali ya kuzama kwa boti ya abiria Mv Baba Philipo iliyotokea Ziwa Tanganyika na iliyokuwa na abiria 110… Mwenyezi Mungu awape pumziko la amani marehemu wote na natoa pole kwa familia kwa kuondokewa na wapendwa wao, serikali iko pamoja nao hasa katika kipindi hiki kigumu na pia tunamuomba mwenyezi Mungu waponye majeruhi wote wa ajali hiyo,” alisema.

Waziri Kamwelwe aliishukuru Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Uvinza ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya, Mwamvua Mrindoko kwa juhudi walizofanya kufika eneo la tukio mapema baada ya kupata taarufa na kusaidia uokozi wa watu na mali.

Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 6:30 mchana Julai 30, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 13 wakiwemo wanawake wawili, wanaume watatu, watoto nane na watu 97 walifanikiwa kuokolewa na pia kumetokea upotevu wa mizigo.

Boti hiyo ilikuwa na usajili namna TKGM 258 ilisajiliwa mwezi Machi 2020 na inamilikiwa na Paulo Mkundya, mkazi wa Uvinza mkoani Kigoma.

Uchunguzi wa awali unaonesha unaonesha kuwa ajali hiyo imetokana na kuzidisha abiria kwa kuwa boti hiyo ilikuwa imeidhinishwa kubeba abiria 50 tu lakini ilibeba abiria zaidi na pia kulikuwa na hali mbaya ya hewa katika eno ilipotokea ajali.

KATIBU Tawala wa Wilaya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi