loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Takukuru Rukwa yaokoa mamilioni ya fedha

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Rukwa imeokoa fedha mbichi kiasi cha Sh 169,828,000 zilizofujwa na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Kuweka na Kukopa (Saccos), miradi ya maendeleo na wakusanyaji sugu wa mapato ya ndani ya halmashauri.

Watoza ushuru sugu wametajwa kuwa ni maofisa watendaji wa vijiji na kata ambao walipewa jukumu la kukusanya mapato ya ndani ya halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga lakini badala ya kuziweka benki walizitafuna.

Hayo yalibanishwa na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Rukwa, Hamza Mwenda alilokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2020 kwa waandishi wa habari.

“Baada ya kufanya ukaguzi katika mradi wa umwagiliaji wa Katongolo wilayani Nkasi na kubaini mkandarasi ambaye ni kampuni ya Girson Investment Ltd alilipwa fedha nyingi kuliko kazi alizotekeleza ... alitemeshwa Sh 45,000,000 ambazo zilirejeshwa kupitia akaunti maalumu ya Mkurugenzi Takukuru iliyoko Benki Kuu ya Tanzania (BOT),” alisema.

Aliongeza kuwa kiasi cha Sh 96,456,250 zimerejeshwa na viongozi wa Saccos mbalimbali na kuwa walimu wastaafu 39 wa Saccos ya Chauwami walirejeshewa Sh 56, 700,000 ambazo zilifujwa na viongozi wao.

“Katika uchunguzi tulioufanya tulibaini uongozi wa Saccos hii walitumia akiba na hisa za wanachama wake kinyume cha Sheria ya Vyama vya Ushirika na 6 ya 2013 ...tuliwabana wakazirejesha zote,” alifafanua.

Aidha taasisi hiyo iliwakabidhi viongozi wa Nkasi Teachers’ Saccos ambazo uongozi wa awali wa Saccos hiyo uliandaa nyaraka na kuwakopesha wasio wanachama kinyume utaratibu.

Aliongeza kuwa kiasi cha Sh 34,212,000 ziliokolewa kutoka kwa wadaiwa sugu ambao walikuwa wakikusanya mapato ya ndani kwa kutumia mashine za kielekroniki (POS) Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.

Aidha taasisi hiyo imeokoa kiasi cha Sh 1,345,000 zilizokuwa za Makupa Saccos iliyopo wilayani Nkasi zilikuwa zimekopeshwa kwa wanachama wake ambao waligoma kuzirejesha kwa mujibu wa utaratibu wa marejesho ya mikopo yao.

Akifafanua alisema kuwa taasisi hiyo imezirejesha fedha hizo kwa uongozi wa Makupa Saccos.

KATIBU Tawala wa Wilaya ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi