loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais muasisi wa Zambia aliyeonja huruma ya Mkapa

WENGI wametoa ushuhuda jinsi Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alivyogusa maisha ya watu wengi ndani na nje ya nchi.

Wakiomboleza kifo chake kilichotokea Julai 23 mwaka huu, watu wengi kupitia majukwaa mbalimbali ikiwamo mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, wana mengi ya kueleza juu ya Mkapa.

Mkapa ambaye alizikwa kijijini kwake Lupaso wilayani Masasi katika mkoa wa Mtwara, ameacha alama nyingi kwa taifa, watu binafsi, taasisi na makundi mbalimbali kama inavyoshuhudiwa na watu wa kada tofauti ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa sifa za Mkapa ambazo waombolezaji walizieleza ni utu, binadamu, ujasiri, huruma, msimamo, weledi, unyenyekevu, ushawishi, ucha Mungu, uchapakazi, upatanishi na usuluhishi.

Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Imakulata Parokia ya Upanga Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Casmir Kavishe alisema Mkapa alipenda aheshimiwe kama muumini wa kawaida na alikuwa hakosi misa kila Jumapili.

Rais John Magufuli katika hotuba yake ya kumuaga jijini Dar es Salaam, alieleza sifa nyingi za Mkapa mojawapo ikiwa ni kuibua vipaji na kuvikuza. Pia Mkapa alisifika kwa misimamo ya kuchukia rushwa na kupenda demokrasia.

Ni orodha ndefu ya watu na taasisi, zinazoeleza sifa za Mkapa alivyogusa maisha yao. Miongoni mwa mashuhuda wanamtaja Rais wa kwanza wa Zambia, Dk Kenneth Kaunda kuwa ni miongoni mwa watu ambao Mkapa aliwasaidia.

“Mengi yamezungumzwa juu ya Mzee Mkapa. Mimi naomba nizungumzie matatu ambayo sijayasikia yakisemwa au pengine hayajasemwa kabisa. Nalo ni moja kuhusiana na usuluhishi,” Balozi wa Tanzania nchini Israel, Job Masima anaeleza kuhusu Kaunda alivyosaidiwa. Anasimulia:

“Mwaka 1997 mimi nilikuwa nikifanya kazi nchini Zambia kama ofisa wa ubalozi. Katika Krismasi ya mwaka huo 1997, serikali ya Zambia ilimkamata aliyekuwa Rais wa kwanza wa nchi hiyo, Mzee Kenneth Kaunda na kumuweka ndani.

“Suala hilo lilizua kizaazaa karibu ulimwengu mzima. Na sote tunajua siwezi kueleza hadithi yote.

Lakini wengi tunajua jinsi Mwalimu Nyerere alivyokuja kuwezesha Mzee Kaunda atoke gerezani. Na katika maisha yake Mwalimu aliingia gerezani katika gereza lililoko mji wa Kabwe nchini Zambia na baadaye Kaunda akatoka.

“Kitu watu wasichofahamu ni kwamba ingawa kweli Mwalimu alikuja na kucheza mchezo wa mwisho, shughuli yote aliifanya Mzee Mkapa. Ndiye alifanya mawasiliano na Rais wa Zambia wakati huo, Frederick Chiluba.

Mzee Mkapa ndiye aliyemtafuta Mwalimu na kumshawishi aingilie kati,” anasema Balozi Masima. Kwa mujibu wa Balozi Masima, Mkapa ndiye aliyemwezesha Mwalimu Nyerere kwa maana ya usafiri na huduma nyingine za kumfikisha mpaka gerezani.

Anasema hiyo ni sifa ya nyongeza ya Mkapa ya kufanikisha kupatanisha viongozi wa nchi moja, waliokuwa na tofauti kutokana na kutoka vyama tofauti. Itakumbukwa mwaka huo ambao Kaunda aliwekwa ndani, Mkapa alikuwa Rais wa Tanzania. Kitabu chake cha ‘My Life, My Purpose’ kinadhihirisha Mkapa alivyokuwa karibu na Mwalimu Nyerere, kwa kueleza alivyomfuata kumfahamisha juu ya azma yake ya kugombea urais na sababu za uamuzi huo.

Katika kitabu hicho, Mkapa aliandika kwamba baada ya kumsikiliza kwa makini Mwalimu Nyerere alimjibu kuwa: “Nitakuwa muwazi kwako. Sikutegemea kuwa ungetaka kuwania urais, wazo kama hilo halikuniingia kabisa.”

Mkapa alishinda uchaguzi mkuu kwa asilimia 61.8 ya kura. Mpinzani wake mkubwa alikuwa Augustino Mrema wakati huo akiwa NCCR-Mageuzi aliyepata asilimia 27.7 ya kura.

Kama alivyosema Balozi Masima, ni dhahiri Mkapa alimwezesha Mwalimu Nyerere kwa maana ya usafiri na huduma nyingine za kumfikisha mpaka gerezani alikokuwa akishikiliwa Kaunda.

Tukio hilo la kukamatwa kiongozi huyo wa zamani wa Zambia, lilirip-otiwa kwa uzito na vyombo mbalimbali duniani hususani alipogoma kula na kunywa akiwa gerezani.

Nyerere alifika mjini Lusaka akiwa ameongozana na mkewe, Mama Maria na kwenda gerezani. Taarifa zinaonesha baada ya kumtembelea na kuzungumza naye, Kaunda alisitisha mgomo huo wa kula.

Vyombo vya habari vilimnukuu Mwalimu Nyerere kwamba walikunywa juisi ya machungwa na kula biskuti ndani ya gereza hilo pamoja na Kaunda, ambaye urafiki wao ulikuwa wa tangu enzi za kupigania uhuru hususani wa nchi Kusini mwa Afrika.

Wakati huo Kaunda alipokamatwa alikuwa na umri wa miaka 73. Alikamatwa baada ya serikali ya Rais Chiluba (sasa marehemu) kumtuhumu kujihusisha na jaribio la mapinduzi la Oktoba.

Kaunda alikana kuwa na uhusiano na askari waliotaka kumpindua Rais Chiluba. Kaunda ni nani? Kaunda mwenye umri wa miaka 96, alizaliwa Aprili 28. Ni rais wa kwanza wa Zambia aliyeingia madarakani Oktoba 24, 1964.

Akiwa na umri wa miaka 40, Kaunda aliongoza Zambia baada ya uhuru kutoka kwa Waingereza. Yeye pamoja na vijana wengine walipambana kuhakikisha nchi inapata uhuru.

Alitoka madarakani Novemba 2, 1991 baada ya Chiluba (sasa marehemu) kuingia madarakani kupitia chama cha Movement for Multiparty Democracy . Chiluba aliingia madarakani baada ya uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi.

Akiwa madarakani, Rais Chiluba alishinda jaribio la kutaka kupinduliwa na wanajeshi waasi na ndipo aliwakamata viongozi kadhaa wa upinzani akiwamo Kaunda akiwatuhumu kuhusika na upangaji njama wa kufanya mapinduzi.

Chiluba aliongoza nchi hiyo hadi mwaka 2001 alipoachia madaraka na nafasi yake kuchukuliwa na Rais Levy Mwanawasa (marehemu) .

Marais wastaafu walivyomuenzi Pamoja na masahibu yaliyomkuta kutokana na siasa za upinzani wakati wa uongozi wa Chiluba, heshima na thamani ya Kaunda maarufu KK inaendelea kuenziwa.

Mwaka jana marais wastaafu kutoka nchi mbalimbali Kusini mwa Afrika, akiwamo Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, walihudhuria sherehe yake ya kutimiza umri wa miaka 95, Aprili 28 iliyofanyika jijini Lusaka.

Wengine wastaafu waliohudhuria ni Rais wa Namibia, Sam Nujoma na Hifikepunye Pohamba; wa Botswana Festus Mogae, Joachim Chissano wa Msumbiji, Bakili Muluzi wa Malawi, Rupia Banda wa Zambia.

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa katika salamu zake za pongezi, alimwelezea Kaunda kuwa ni rais mwanzilishi wa Zambia na shujaa wa ukombozi wa nchi hiyo.

Kwenye salamu zake alizomtumia kupitia ubalozi wa Zambia uliopo Pretoria, Ramaphosa alimtaja Kaunda kuwa ni shujaa, asiye na ubinafsi, aliyepigana dhidi ya mabeberu, ukoloni na ubaguzi wa rangi ambaye juhudi zake zilichangia pia uhuru wa kisiasa kwa Afrika Kusini na nchi nyingine za ukanda.

“Ziara ya marais wastaafu ni ya kihistoria na kiashiria cha kutambua mchango mkubwa aliotoa Kaunda katika ukombozi Kusini mwa Afrika,” ndivyo Balozi wa Zambia nchini Afrika Kusini, Emmanuel Mwamba alivyokaririwa akisema kupitia vyombo vya habari.

Mwaka jana, Kaunda pia alitunukiwa tuzo kwa juhudi zake za kuboresha uwazi na kupambana na rushwa. Tuzo hiyo ilitolewa katika sherehe zilizofanyika jijini Kigali nchini Rwanda.

Hata hivyo, Kaunda hakuweza kwenda nchini humo. Badala yake, binti yake mdogo, Cheswa Silwizya, ndiye alikwenda kumwakilisha. Wasifu wake Kaunda ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanane.

Alizaliwa katika Hospitali ya Misheni ya Lubwa katika kitongoji cha Chinsali Mkoa wa Magharibi mwa nchi hiyo ya Zambia, ambayo wakati huo ilijulikana kama Rhodesia ya Kaskazini. Baba yake, David Kaunda, alikuwa kiongozi wa Kanisa la Kiskoti na mwalimu wa shule za wamisionari.

Mama yake pia alikuwa mwalimu. Alizaliwa nchini Malawi na kuhamia Chinsali kwa lengo la kufanya kazi katika misheni ya Lubwa. Kaunda alipata elimu na kuhitimu sekondari miaka ya 1940.

Kama ilivyo kwa Waafrika waliokuwa wakati wa ukoloni, pia Kaunda alianza kufundisha nchini humo na baadaye alifundisha nchini Tanganyika (sasa Tanzania).

Alirudi Zambia mwaka 1949. Alipata uzoefu kuhusu serikali ya kikoloni na masuala ya siasa, ambayo yalimsaidia baadaye alipojiunga na Chama cha African National Congress (ANC), ambacho kilikuwa chama cha kwanza cha kupigania uhuru. Mwanzoni mwa mwaka 1950 Kaunda alikuwa Katibu Mkuu wa ANC.

Kaunda ni muasisi pekee wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) aliye hai. Wakati mwezi ujao jumuiya hiyo inatarajwa kuadhimisha miaka 40 tangu kuundwa kwake, Kaunda ataalikwa akiwa ni muasisi pekee.

Machi mwaka huu Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya SADC, Dk Stergomena Tax akitoa maazimio ya Baraza la Mawaziri wa jumuiya, alisema Kaunda atakaribishwa kwenye sherehe hizo zitakazofanyika Msumbiji, Agosti mwaka huu.

Jumuiya hiyo ilizaliwa kutokana na Jukwaa la Kuratibu Harakati za Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADCC) ambalo rais huyu mstaafu alikuwa muasisi. Ni muasisi tangu kuanza kwa harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika kupitia Klabu ya Marais ya Mulungushi, Nchi za Mstari wa Mbele (FLS) na SADCC iliyozaa SADC.

Marais wengine waasisi ni Mwalimu Nyerere, Seretse Khama wa Botswana, Antonio Neto wa Angola, Samora Machel wa Msumbiji na Dk Kamuzu Banda wa Malawi.

Huyu ndiye Kaunda ambaye jina lake liko sambamba na la Nyerere zinapotajwa harakati za ukombozi kusini mwa Afrika. Ndiyo maana Nyerere aliamua kwenda kumtembelea gerezani na kufanikisha kumtoa huku Rais Mkapa akiwa sehemu ya uwezeshaji huo kama simulizi ya Balozi Masima inavyosema.

Iliripotiwa kwa uzito na vyombo mbalimbali duniani hususani alipogoma kula na kunywa akiwa gerezani. Nyerere alifika mjini Lusaka akiwa ameongozana na mkewe, Mama Maria na kwenda gerezani.

Taarifa zinaonesha baada ya kumtembelea na kuzungumza naye, Kaunda alisitisha mgomo huo wa kula. Vyombo vya habari vilimnukuu Mwalimu Nyerere kwamba walikunywa juisi ya machungwa na kula biskuti ndani ya gereza hilo pamoja na Kaunda, ambaye urafiki wao ulikuwa wa tangu enzi za kupigania uhuru hususani wa nchi Kusini mwa Afrika.

Wakati huo Kaunda alipokamatwa alikuwa na umri wa miaka 73. Alikamatwa baada ya serikali ya Rais Chiluba (sasa marehemu) kumtuhumu kujihusisha na jaribio la mapinduzi la Oktoba.

Kaunda alikana kuwa na uhusiano na askari waliotaka kumpindua Rais Chiluba.

Kaunda ni nani?

Kaunda mwenye umri wa miaka 96, alizaliwa Aprili 28. Ni rais wa kwanza wa Zambia aliyeingia madarakani Oktoba 24, 1964. Akiwa na umri wa miaka 40, Kaunda aliongoza Zambia baada ya uhuru kutoka kwa Waingereza.

Yeye pamoja na vijana wengine walipambana kuhakikisha nchi inapata uhuru. Alitoka madarakani Novemba 2, 1991 baada ya Chiluba (sasa marehemu) kuingia madarakani kupitia chama cha Movement for Multiparty Democracy .

Chiluba aliingia madarakani baada ya uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi. Akiwa madarakani, Rais Chiluba alishinda jaribio la kutaka kupinduliwa na wanajeshi waasi na ndipo aliwakamata viongozi kadhaa wa upinzani akiwamo Kaunda akiwatuhumu kuhusika na upangaji njama wa kufanya mapinduzi.

Chiluba aliongoza nchi hiyo hadi mwaka 2001 alipoachia madaraka na nafasi yake kuchukuliwa na Rais Levy Mwanawasa (marehemu) .

Marais wastaafu walivyomuenzi Pamoja na masahibu yaliyomkuta kutokana na siasa za upinzani wakati wa uongozi wa Chiluba, heshima na thamani ya Kaunda maarufu KK inaendelea kuenziwa.

Mwaka jana marais wastaafu kutoka nchi mbalimbali Kusini mwa Afrika, akiwamo Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, walihudhuria sherehe yake ya kutimiza umri wa miaka 95, Aprili 28 iliyofanyika jijini Lusaka.

Wengine wastaafu waliohudhuria ni Rais wa Namibia, Sam Nujoma na Hifikepunye Pohamba; wa Botswana Festus Mogae, Joachim Chissano wa Msumbiji, Bakili Muluzi wa Malawi, Rupia Banda wa Zambia.

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa katika salamu zake za pongezi, alimwelezea Kaunda kuwa ni rais mwanzilishi wa Zambia na shujaa wa ukombozi wa nchi hiyo.

Kwenye salamu zake alizomtumia kupitia ubalozi wa Zambia uliopo Pretoria, Ramaphosa alimtaja Kaunda kuwa ni shujaa, asiye na ubinafsi, aliyepigana dhidi ya mabeberu, ukoloni na ubaguzi wa rangi ambaye juhudi zake zilichangia pia uhuru wa kisiasa kwa Afrika Kusini na nchi nyingine za ukanda.

“Ziara ya marais wastaafu ni ya kihistoria na kiashiria cha kutambua mchango mkubwa aliotoa Kaunda katika ukombozi Kusini mwa Afrika,” ndivyo Balozi wa Zambia nchini Afrika Kusini, Emmanuel Mwamba alivyokaririwa akisema kupitia vyombo vya habari.

Mwaka jana, Kaunda pia alitunukiwa tuzo kwa juhudi zake za kuboresha uwazi na kupambana na rushwa. Tuzo hiyo ilitolewa katika sherehe zilizofanyika jijini Kigali nchini Rwanda.

Hata hivyo, Kaunda hakuweza kwenda nchini humo. Badala yake, binti yake mdogo, Cheswa Silwizya, ndiye alikwenda kumwakilisha.

Wasifu wake Kaunda ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanane. Alizaliwa katika Hospitali ya Misheni ya Lubwa katika kitongoji cha Chinsali Mkoa wa Magharibi mwa nchi hiyo ya Zambia, ambayo wakati huo ilijulikana kama Rhodesia ya Kaskazini.

Baba yake, David Kaunda, alikuwa kiongozi wa Kanisa la Kiskoti na mwalimu wa shule za wamisionari.

Mama yake pia alikuwa mwalimu. Alizaliwa nchini Malawi na kuhamia Chinsali kwa lengo la kufanya kazi katika misheni ya Lubwa. Kaunda alipata elimu na kuhitimu sekondari miaka ya 1940.

Kama ilivyo kwa Waafrika waliokuwa wakati wa ukoloni, pia Kaunda alianza kufundisha nchini humo na baadaye alifundisha nchini Tanganyika (sasa Tanzania).

Alirudi Zambia mwaka 1949. Alipata uzoefu kuhusu serikali ya kikoloni na masuala ya siasa, ambayo yalimsaidia baadaye alipojiunga na Chama cha African National Congress (ANC), ambacho kilikuwa chama cha kwanza cha kupigania uhuru. Mwanzoni mwa mwaka 1950 Kaunda alikuwa Katibu Mkuu wa ANC.

Kaunda ni muasisi pekee wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) aliye hai. Wakati mwezi ujao jumuiya hiyo inatarajwa kuadhimisha miaka 40 tangu kuundwa kwake, Kaunda ataalikwa akiwa ni muasisi pekee. Machi mwaka huu Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya SADC, Dk Stergomena Tax akitoa maazimio ya Baraza la Mawaziri wa jumuiya, alisema Kaunda atakaribishwa kwenye sherehe hizo zitakazofanyika Msumbiji, Agosti mwaka huu. Jumuiya hiyo ilizaliwa kutokana na Jukwaa la Kuratibu Harakati za Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADCC) ambalo rais huyu mstaafu alikuwa muasisi.

Ni muasisi tangu kuanza kwa harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika kupitia Klabu ya Marais ya Mulungushi, Nchi za Mstari wa Mbele (FLS) na SADCC iliyozaa SADC.

Marais wengine waasisi ni Mwalimu Nyerere, Seretse Khama wa Botswana, Antonio Neto wa Angola, Samora Machel wa Msumbiji na Dk Kamuzu Banda wa Malawi.

Huyu ndiye Kaunda ambaye jina lake liko sambamba na la Nyerere zinapotajwa harakati za ukombozi kusini mwa Afrika. Ndiyo maana Nyerere aliamua kwenda kumtembelea gerezani na kufanikisha kumtoa huku Rais Mkapa akiwa sehemu ya uwezeshaji huo kama simulizi ya Balozi Masima inavyosema.

OKTOBA 28, 2020 Tanzania itafanya Uchaguzi Mkuu kuchagua rais, wabunge ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi