loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Harmonize asajili kimataifa

MSANII na mmiliki wa lebo ya Konde Gang Music, Rajab Abdul ‘Harmonize’ amemtangaza msanii mpya kwenye lebo yake kutoka nchini Nigeria aitwaye Raoul John ‘ Skales’.

Harmonize alimtangaza msanii huyo jana kupitia ukurasa wake wa Instagram, na anakuwa msanii wa pili kujiunga na lebo hiyo. Pia Harmonize alitumia ukurasa huo huo wa Instagram kusema:

“Ni ndoto za muziki wa Afrika kwenda duniani, tunayo furaha kumkaribisha msanii mwenye akili na kipaji kutoka Nigeria, kaka yangu, Young Skales kwenye familia ya Konde Gang, hii ni timu ya ndoto”.

Skales ataungana na msanii mwenziye, Ibraah Tz ambao watakuwa pamoja kwenye lebo ya Konde Gang. Skales amewahi kushirikiana na Harmonize kwenye nyimbo kama Fire West, Oliver Twist Remix, Oyoyo na Rumba.

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wametajwa katika tetesi ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi