loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Binadamu kubadili DNA ili kuishi Mars

WANASAYANSI wanasema kama binadamu anataka kwenda kuishi katika sayari ya Mars ni lazima aondokane na ubinadamu wake duniani.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni Shirika la Utafiti wa Anga za Juu la Marekani (NASA) likijiandaa na safari ya kwanza ya kupelekwa wanadamu katika sayari hiyo miaka ya 2030.

Imeelezwa wanaanga watakaoweza kufika sayari hiyo na kuishilazima wawe wana uwezo wa kupambana na minururisho mikali, upotevu wa uwezo wa mifupa katika nguvu ndogo za mvutano na athari nyingine zinazofuatana nayo.

Wanasayansi hao wamesema kuwa watu hao wanaweza kurejea nyumbani (duniani) wakiwa wazima licha ya hekaheka watakazokuta huko. Ingawa wanaorudi wanaweza kuwa katika hali bora, wanaobaki huko, watatakiwa kubadilishwa baadhi ya mambo ya msingi katika ubinadamu wao kwani hawawezi kuishi huko wakiwa wamebakisha vinasaba vyao vya msingi sasa.

Wataalamu wanasema hali aliyonayo binadamu hapa duniani, haiwezi kumwezesha kuishi Mars lakini anaweza kama vinasaba vyake DNA vitabadilishwa kukabili mazingira ya Mars.

Mtaalamu wa baiolojia ya anga za juu, Kennda Lynch, ambaye pia ni mbaiolojia wa miamba kituo cha sayansi za anga za juu cha Lunar and Planetary Institute cha mjini Houston, alisema mazingira ya kufanya makazi Mars ni magumu hadi vitu vya msingi kwa binadamu vibadilike.

Aidha, alisema hilo linawezekana kwa kuwa utaalamu uhandisi wa vinasaba upo juu sasa. Uhandisi wa vinasaba umekuwa ukizungumzwa na watunzi wa vitabu vya simulizi za kisayansi.

Imeelezwa hata hivyo kwamba majaribio yameshaanza ya kubadili DNA ya binadamu ili kukabiliana n tatizo la minururisho ya hatari. Maelezo hayo yalitolewa na Christopher Mason, mtaalamu wa vinasaba wa Shule Kuu ya Weill Cornell Medicine ya Chuo Kikuu cha Cornell mjini New York City, nchini Marekani.

NASA wamesema wameshaanza kuchukua hatua za kuhami vinasaba vya wana anga wao na kila kitu kinachohusu usalama wao kimeanza kushughulikiwa kabla ya safari miaka ijayo.

Uhandisi wa vinasaba umeelezwa kuwa hatua kubwa mbele, wanaysayansi wakiwa na uwezo wa kutengeneza vinasaba wanavyovitaka kwa ajili ya kupeleka binadamu sayari ya Mars.

Pia katika ghuba ya eneo hilo iko Iran, hasimu wa UAE iliyowekewa vikwazo na Marekani kufuatia mpango wake tatanishi wa nyuklia. Warusi waongeza utafutaji taarifa kuhusu Tanzania Binadamu kubadili DNA ili kuishi Mars Roketi kubwa la Atlas V likichupa hewani kusindikiza chombo maalumu (NASAPersevere ) kinachomilikiwa na Taasisi ya Utafiti wa Anga za Juu ya Marekani (NASA) kwenda kuchunguza uhai katika sayari ya Mars .

Chombo hicho ambacho ndani yake pia kimebeba helkopta kinategemewa kusafiri kwa miezi saba na kufika kreta ya Jezero, Mars Februari 18,2021. Perseverance kitakuwa chombo cha tano kutumwa na NASA kwenye sayari ya Mars.

Vyombo vingine ni Sojourner, Spirit, Opportunity na Curiosity.Urushaji wa chombo hicho ulifanyika kwa ufanisi mkubwa katika kitua Kituo cha Jeshi la Anga la Marekani cha Cape Canaveral, Florida.( Picha na Xinhua).

MOSCOW, Urusi URUSI imebaini kuwa Marekani imekuwa ikitoa msaada kwa waandishi wa habari, taasisi za elimu na asasi zisizo za kiserikali katika nchi za Afrika kwa kutengeneza madai ya uongo dhidi ya Urusi kwenye vyombo vya habari.

Katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, msemaji wa wizara hiyo, Maria Zajharova alisema kwa kisingizio cha kuongeza uwazi wa taasisi za serikali na kuongeza utulivu wa mfumo wa Mahakama Afrika, Marekani imekuwa ikigharimia juhudi za kutafuta mabaya ya Urusi.

“Kwa jinsi ninavyoona, hali ya sasa nchini Marekani si bora kusaidia Afrika, inatakiwa ianze kujisaidia yenyewe kwanza kwani ina mambo mengi inapaswa kufanya,” alisema.

Alibainisha Urusi haina jinsi zaidi ya kutoa maoni na kuelezea kwa nini inaona kama Marekani inajitahidi kuondoa msingi mzuri wa kisiasa na kijamii kwa Urusi. Nchi hiyo ilionekana wazi kufuatilia Mkutano wa Urusi na Afrika uliofanyika Sochi Oktoba, mwaka jana.

foto
Mwandishi: HOUSTON, Marekani

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi