loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maambukizi corona yafikia 700 kwa siku

KENYA inaendelea kutaabika kutokana na maambukizi ya virusi vya corona na kufi kia kiwango cha juu katika kipindi cha saa 24.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya nchi hiyo, maambukizi ya virusi hivyo yamefikia 700 kila baada ya saa 24, huku idadi ya kaunti zilizoathiriwa ikiongezeka kutoka 44 hadi 46, ikibaki moja tu kufikisha idadi ya kaunti zote zinazounda Jamhuri ya Kenya.

Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona nchini humo inaelezwa imekuwa ya juu katika kipindi cha siku tano mfululizo.

“Katika kipindi kilichopita cha takribani siku tano mfululizo kumekuwa na ongezeko kubwa la wastani wa wagonjwa wanaoripotiwa katika sehemu mbalimbali nchini humo, ambapo katika kipindi cha saa 24 katika kila siku ya siku hizo tano kumeripotiwa wastani wa wagonjwa 695,” ilisema taarifa ya Wizara ya Afya.

Jumapili wizara hiyo ilitangaza kuwa wagonjwa walioripotiwa hospitalini na kupimwa na kukutwa na ugonjwa wa covid-19 ni 690 na idadi hiyo inatokana na upimaji mkubwa uliofanywa na maofisa wa afya.

Hadi kufikia Jumapili, Kenya ilikuwa ina wagonjwa 22,053wa covid-19 ikipaa na kushika nafasi ya tano barani Afrika, ikiongozwa na Afrika Kusini yenye maambukizi zaidi ya 500,000.

Kati ya wagonjwa hao 690, jiji la Nairobi liliongoza kwa kuwa na wagonjwa 535, Kiambu 56, Kajiado 28, Nyeri 24, Busia 9, Machakos 7, Nakuru na Kisumu 6 kila moja na Embu na Garissa 4 kila moja.

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi