loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakulima wa tumbaku waishitaki serikali

WAKULIMA zaidi ya 500 wa zao la biashara la tumbaku wameipeleka serikali mahakamani kutokana na suala la malimbikizo ya fedha zao za mauzo.

Wakulima hao wameishitaki kampuni ambayo ndiyo mdhamini wao ya Continental Tobacco Company inayomilikiwa na serikali.

Sababu za kushitakiwa kwa kampuni hiyo ni kutokana na kushindwa kuwalipa wakulima hao Sh bilioni mbili za Uganda, ikiwa ni gharama za kuiuzia tumbaku.

Shauri hili limewasilishwa katika Mahakama ya kiraia, ambapo wakulima hao wakiongozwa na Godfrey Tinkasimire, wakimshitaki mwanasheria mkuu wa serikali kama mtu wa mwisho anayetoa leseni au ruhusa ya malipo kufanyika.

Wakulima hao pia wamemshitaki mwanasheria mkuu wa serikali kwa kushindwa kulinda maslahi ya wakulima wa zao la tumbaku kwa kuhakikisha kuwa mali na fedha zao zinakuwa salama na wanapata haki zao.

Kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa na wakulima hao na serikali, walitakiwa kulima tumbaku kama watakavyoshauriwa na kampuni ya kahawa lakini wasiuze kwa kampuni nyingine.

Kampuni hiyo ya kahawa ndiyo mnunuzi, mchakataji na mzalishaji wa mazao ya tumbaku kwa mwaka 2017/2018, 2018/2019 na 2019/2020.

foto
Mwandishi: KAMPALA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi