loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mashirika zaidi kutua KIA kunaonesha kuaminika kwa Tanzania

KUMEKUWAPO na habari za kufurahisha kuhusu mashirika zaidi ya ndege kuanza kutua tena katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) baada ya kipindi kirefu cha dunia kuhangaika na ugonjwa wa covid-19.

Ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya corona ulisababisha anga za nchi mbalimbali kufungwa na kusababisha biashara ya kusafirisha mizigo na abiria kwa njia ya anga kukwama.

Hali hiyo pia iliua shughuli mbalimbali zinazogusa sekta ya utalii na kilimo cha mboga na matunda na kufanya shughuli za uchumi zinazowezeshwa na uwapo wa huduma hiyo kuyumba.

Ndio kusema taarifa kwamba Shirika la Ndege la Rwanda, Rwandair, limefanya safari na kutua KIA kwa kutumia ndege yake aina ya 9XR- WL ni taarifa njema kwa kuwa sasa, rasmi nchi hizi mbili zinaweza kutumia anga lake kwa ajili ya shughuli za kibiashara.

Pamoja na kupongeza uamuzi wa shirika hilo kurejesha safari zake nchini Tanzania na kuanza kutua KIA, uamuzi huo ni wa kupongezwa na jamii ambayo kukosekana kwa huduma hiyo ya anga kulikuwa kunavuruga ustawi wa wananchi wa pande zote mbili hasa ukizingatia kutegemeana kwa nchi hizo mbili zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tunaupongeza uongozi wa Kampuni ya Uendeshaji na Uendelezaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kadco), kwa juhudi zake kubwa za kushawishi utumiaji wa uwanja wa huo.

Tunatambua kwamba kwa juhudi za Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kadco, Christine Mwakatobe, watendaji na wafanyakazi wa kampuni hiyo tayari mashirika manne ya ndege yanatua katika uwanja huo.

Tumekuwa tukishuhudia kuanzia Juni Mosi, mwaka huu Kadco wakipokea ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, Ethiopian Airline, Julai 30 wakipokea ndege ya Qatar Airline, Agosti Mosi, shirika la Crystal na Shirika la Ndege la Uholanzi, KLM ; hali hiyo inaonesha kuanza kurejea kwa hali ya kawaida katika mahusiano ya kimataifa na ujio wa jirani umekuwa na faida kubwa kwa pande zote mbili.

Ni dhahiri kwamba, uamuzi wa mashirika ya ndege kuanza tena safari kuja nchini, umeonesha namna walivyoridhishwa na jinsi Tanzania ilivyokabili ugonjwa wa covid-19.

Tunawapongeza Watanzania na serikali kwa kufanikisha mapambano dhidi ya covid-19 ambapo mafanikio yake ni kwa nchi kuwa eneo shwari na salama kuwezesha maisha kuendelea kama kawaida.

Tuna amini juu ya kauli ya Meneja wa Rwandair, Jammy Mitali, kwamba shirika hilo limerudisha safari zake Tanzania baada ya kuona hakuna tishio la ugonjwa wa covid 19.

HATIMAYE safari za ndege kati ya Tanzania na Kenya zimerejea ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi