loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Urusi yaionya Marekani usambazaji wa mabomu

URUSI imesema itajibu vikali kitendo cha Marekani kusambaza makombora yake ya masafa marefu na masafa ya kati katika maeneo mbalimbali duniani.

Hayo yalibainishwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi mwanzoni mwa wiki hii.

“Ni wazi kwamba usambazaji wa makombora ya masafa mafupi na masafa ya kati ya Marekani duniani, kwa kiasi kikubwa unadhoofisha usalama wa kikanda na kiulimwengu na utachochea awamu mpya ya hatari ya matumizi ya silaha,” ilisema Wizara hiyo na kuongeza;

“Urusi haiwezi kupuuzia kuonekana kwa vitisho zaidi vya makombora kwa ardhi yake ambayo inaonekana ni ya kimkakati kwetu.

Jambo hili litahitaji kujibiwa haraka bila kujali ni makombora gani yatakayosambazwa iwe nyuklia au la.

” Wizara hiyo ilibainisha kuwa hatua pekee na muhimu kwa sasa ni kuangalia kwa pamoja namna ya kupata ufumbuzi wa suala hilo kwa njia za kisiasa na kidiplomasia.

“Urusi itaendelea kuwa wazi kwa jukumu la kujenga na kurejesha imani na kuimarisha usalama wa kimataifa na utulivu. Tunatazamia kuwepo kwa uwajibikaji kama huo kwa upande wa Marekani,” ilisema Wizara hiyo.

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi