loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dawa kupambana na corona yasambazwa

URUSI imeanza kusambaza dawa aina ya Avifavir ya kupambana na virusi vya corona katika nchi zaidi ya 15. Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mfuko wa Uwekezaji (RDIF), Kirill Dmitriev.

Dmitriev alisema dawa hiyo imesambazwa kwa nchi za Latin Amerika na Afrika Kusini, lakini pia katika nchi jirani. Uuzaji wa dawa hiyo ya kupambana na Covid-19 unafanywa na Kampuni ya Chromis ambayo ilianzishwa kwa ubia kati ya RDIF na ChemRar Group.

Alisema Avifavir ni miongoni mwa dawa mbili za Covid-19 zilizosajiliwa duniani.

Dawa hiyo ya kunywa ni ya kwanza duniani kuidhinishwa kutibu ugonjwa wa Covid-19 na imeonesha ufanisi mkubwa katika majaribio ya kliniki kwa kuharibu mfumo wa kujizalisha virusi vya corona.

Dawa hiyo ilipata cheti cha usajili kutoka Wizara ya Afya ya Urusi Mei 29 mwaka huu na kuwa dawa ya kwanza ya Urusi iliyoidhinishwa kutibu wagonjwa wa Covid-19.

Aidha Juni 3 mwaka huu, Wizara ya Afya nchini humo iliijumuisha Avifavir katika toleo la saba la miongozo ya kuzuia, kutambua na kutibu maambukizi ya virusi vya corona.

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi