loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Petroli, dizeli bei juu

MAFUTA aina ya petroli yamepanda bei kwa Sh 139 sawa na asilimia 8.22 na dizeli imepanda bei kwa sh 69 sawa na asilimia nne.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Titus Kaguo aliyasema hayo jana jijini Dodoma na kubainisha kuwa bei hizo zinaanza kutumika leo.

Kaguo alisema kuwa petroli mkoani Dar es Salaam, itauzwa kwa Sh 1,832 na dizeli itauzwa sh 1,785.

“Hivyo kama wewe ni mkazi wa Dodoma unatakiwa kuchukua bei inayotumika sasa na kujumlisha na sh 139 ili kupata bei mpya ya petroli na vile vile kwa upande wa dizeli unajumuisha na shilingi 69” aliswema.

Kaguo alisema kuwa bei zimeongezeka kutokana na matumizi na mahitaji ya watu kuongezeka baada kwisha ugonjwa wa Covid-19 tofauti na miezi ya nyuma wakati waagizaji walipoagiza kidogo kwa hofu baada ya kusambaa virusi vya corona.

Alisema kuwa petroli iliyoingia kupitia bandari ya Tanga, imepanda kwa Sh 214 sawa na asilimia 12.94 na dizeli imepanda kwa Sh 85 katika mkoa wa Tanga sanjari na mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

Petroli iliyoingia kupitia bandari ya Mtwara ilipanda kwa Sh 263 na dizeli kwa Sh 68 na hivyo inaonesha mabadiliko hayo hayapishani sana katika bandari hizo pamoja na Dar es Salaam.

Meneja wa Biashara Kitengo cha Petroli, Kemilembe alisema kuwa Bandari ya Tanga ilipokea mafuta Aprili ambayo yameanza kutumika Mei na hivyo bei imepanda kidogo kulingana na bei ya soko la dunia wakati huo.

Bandari ya Mtwara ilipokea petroli Machi na bei ilianza kutumika Aprili na hivyo kuleta mabadiliko ya bei. Meneja Uchambuzi wa Mahesabu ya Kifedha Ewura, Msafiri Mtepa alisema upangaji wa bei huzingatia kanuni na taratibu na wafanyabiashara wanazifahamu kanuni hizo.

Kaguo alisema kuwa hakuna tatizo la mafuta nchini, kwa kuwa kuna meli sita zitaingiza mafuta ya petroli nchini kati ya Julai 29 na Agosti 31 mwaka huu. Alisema meli tatu zimewasili nchini zikiwa na jumla ya lita milioni 89.564 kwa ajili ya soko la ndani na kiasi hicho kitatosheleza kwa siku 18.

Meli nyingine tatu zitawasili kati ya Agosti 17-31 mwaka huu zikiwa na takribani lita milioni 100.075, zitakazotosheleza mahitaji ya nchi kwa zaidi ya siku 22. Kuhusu mafuta ya dizeli, alisema kuwa yapo ya kutosha na meli tatu za mafuta zenye jumla ya lita milioni 193.391, zinatarajiwa kuwasili nchini mwezi huu.

Mafuta hayo yatatosheleza mahitaji ya dizeli kwa zaidi ya siku 30. Kuhusu usambazaji wa mafuta, alisema kuwa kanda zote nchini zina mafuta. Alisema kuwa changamoto zilizopatikana kwa petroli Julai mwaka huu, imechangiwa na uchelewaji wa meli moja iliyokuwa ifike kati ya Julai 22 na 24 ilifika Julai 29.

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

1 Comments

  • avatar
    isaka mwasote
    05/08/2020

    kwa maelezo au habari nilivo isoma kwa kweli serikali iko makini kwa utekelezaji wa huduma kwa wananchi mbarikiwe.......lakini naamini katika kujenga taifa nadhani mnapaswa kupongezwa lakini mshukuliwe kwa kutuwekea app hii tunainjoi kupata taarifa kwa haraka note: uzalendo na uhuru kwanza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi