loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yaongeza siku 2 Maonesho Nanenane

SERIKALI imeongeza siku mbili za maadhimisho ya Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi maarufu Nanenane kwa mwaka huu kutokana na baadhi ya kanda za maonesho kuchelewa kuanza maoneshoo hayo.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (pichani) alipotembelea banda la Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania(TABWA) katika maonesho hayo, yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu kwenye viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi.

Alisema kuwa kulingana na mahitaji ya sherehe za wakulima kujifunza mbinu bora za kilimo, wananchi ambao hawakupata fursa siku za mwanzo wa maonesho hayo ambayo yalizinduliwa Agosti mosi mwaka huu, watapata nafasi ya siku hizo mbili zilizoongezwa kujionea mbinu bora za kilimo, mifugo na uvuvi.

Awali maonesho hayo yalifunguliwa Agosti mosi mwaka huu na kilele itakuwa Agosti 8, lakini kwa kauli hiyo ya Waziri Hasunga, maonesho hayo yatafungwa Agosti 10,mwaka huu katika kanda zote.

Alisema malengo makubwa ya maonesho hayo ni kuwaunganisha wakulima, wafugaji, wavuvi na wanaushirika, kusherehekea kwa pamoja ikiwemo kuonesha teknolojia ya zana bora za kilimo, mifugo na Uvuvi.

Hasunga alisema maonesho hayo yanatoa fursa ya kuwakutanisha wakulima, wavuvi na wafugaji na watoa huduma za fedha, bima, mawasiliano, taasisi za umma na binafsi.

Maeneo ambayo maonesho hayo yanafanyika ni kwenye kanda saba ambazo ni Mwanza, Tabora, Simiyu, Mbeya, Dodoma, Morogoro, Arusha na Lindi. Katika maonesho hayo wakulima, wafugaji na wavuvi wanahamasishwa kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ambapo wametakiwa kuchagua viongozi bora wenye uwezo wa kuendeleza kilimo.

Maonesho hayo yanachagizwa na Kauli mbiu isemayo “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Chagua Viongozi Bora 2020”.

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick, Bariadi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi