loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bale kuamua usajili wa Real Madrid

BAADA ya Madrid kutwaa ubingwa wa La Liga mwezi uliopita, Rais Florentino Perez, amethibitisha hakuna usajili mkubwa utakaofanyika kutokana na madhara ya virusi vya corona.

Lakini vyanzo vya habari vya klabu viliiambia ESPN kwamba, kuondoka Bale, 31, kutawafanya kufanya usajili mwingine. Maofisa wakongwe kwenye klabu wana amini hali ya kifedha ilivyo kwa sasa inakuwa ngumu kufanya usajili mkubwa.

Real Madrid imeshindwa taji la 34 la La Liga Julai 16 baada ya kushinda mara 10 mfululizo na kumzidi mpinzani wake Barcelona kwenye msimamo. Mshambuliaji huyo wa Wales ameanza mara moja akiwa mchezaji wa akiba baada ya La Liga kurejea tena Juni na kuachwa kwenye mechi zote za msimu zilizosalia, huku kocha Zinedine Zidane, akisema kukosekana kwake ni kutokana na maamuzi ya kiufundi.

Licha ya wawili hao kuonekana wenye matatizo, baadhi ya maofisa Bernabeu wanaamini hilo linaweza kuwekwa sawa wakimtafsiri Bale kuwa na uwezo wa kufunga jambo linalokosekana kwenye kikosi cha sasa cha Real Madrid. Aidha, klabu hiyo ipo tayari kumuacha Bale aondoke msimu huu baada ya mpango wa kwenda China mwaka jana kukwama.

Majadiliano kuhusu kumuuza yanamkanganyiko, kwa mujibu wa chanzo cha ESPN, kwani timu kadhaa haziko tayari kukabiliana na mshahara wa Bale na Madrid haipo tayari kumuuza kwa bei ya kutupa mchezaji wa aina ya Bale.

Vyanzo vya karibu na Bale vinaendelea kusisitiza kwamba, ana furaha Madrid na anajipanga kuona namna atakavyomaliza mkataba wake unaotarajiwa kumalizika 2022.

MIKEL Arteta amesema hakuumizwa na kipigo cha Arsenal timu yake ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi