loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Lewandowski ammwagia sifa luluki Klopp

MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich, Robert Lewandowski, amesema anadhani kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, ana sura mbili, moja kocha na nyingine baba.

Lewandowski, 31, amecheza misimu minne chini ya Klopp Borussia Dortmund kabla ya wawili hao kuhama timu tofauti. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland amesema, Mjerumani huyo ni kocha anayempenda kati ya wote aliocheza chini yao.

“Nadhani Jurgen Klopp (Kocha ninayempenda) baada ya Pep Guardiola. Asilimia 100. (Klopp) ana sura mbili, unaweza kumuona kama baba, lakini pia ni kocha, anaweza kukwambia kila kitu na sizungumzi kuhusu vitu vyake vizuri ama vibaya.”

“Pia kwa wachezaji, ni mwenye kutoa hamasa, anafanya vizuri kwa sababu anajua wapi akukazanie uongeze jitihada.” “Anapokuwa kocha utampenda, lakini sio kwenye ukocha tu, hata kwenye kuwa baba,” alisema.

Lewandowski ameendelea kuwa mmoja wa wafungaji bora duniani tangu ajiunge na mabingwa mara nane wa Bundesliga, akifunga mabao 51 katika mechi 43 msimu huu, ikiwamo mabao 34 kwenye ligi kuu na kuifanya Bayern ishinde ubingwa wa ligi na kombe la ligi.

Mechi inayofuata kwa Bayern ni ile ya marudiano ya hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Chelsea mwishoni mwa wiki hii ambapo timu ya Lewandowski iko mbele kwa mabao 3-0 iliyoyapata katika mechi ya kwanza kabla ya kwenda kwenye mapumziko ya miezi mitatu yaliyotokana na virusi vya corona.

Aidha, Lewandowski hakutaka kujiaminisha kufanya vizuri katika mechi hiyo licha ya kuwa kwenye nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali mjini Lisbon. “Chelsea inacheza vizuri. Lakini sina wasiwasi, najua sisi ni Bayern Munich na tunaiheshimu Chelsea. Najua tupo kwenye kiwango kizuri na tunajua kilichotokea kwenye mechi ya kwanza.” “Tunahitaji kuwa na dakika 20 nzuri za mwanzo, lakini tupo vizuri baada ya mapumziko (Tangu Bundesliga ilipoisha),” alisema Lewandowski.

MIKEL Arteta amesema hakuumizwa na kipigo cha Arsenal timu yake ...

foto
Mwandishi: MUNICH, Ujerumani

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi