loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DC amshukuru JPM kuboresha sekta ya afya

MKUU wa Wilaya ya Kibaha, Martin Ntemo, amemshukuru Rais John Magufuli, kwa kuipatia wilaya hiyo Sh bilioni 2.7 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya kwenye vituo vitatu vya afya vya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.

Aliyasema hayo kwenye kitongoji cha Disunyala, Mlandizi, Kibaha, wakati wa uzinduzi wa utoaji huduma katika kituo kipya cha afya cha wilaya hiyo juzi.

Alisema kupatikana kwa fedha hizo kutasababisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.

Ntemo alisema kati ya fedha hizo, Sh bilioni 1.8 zimetumika kwenye ujenzi wa kituo hicho ambacho kina majengo saba kwa hatua ya kwanza, huku Sh milioni 500 zikitu mika kwa ajili ya upanuzi wa kituo cha afya Magindu na Sh milioni 400 zimetumika kukarabati kukarabati kituo cha afya Mlandizi.

“Leo (jana) tumezindua utoaji wa huduma za afya kwenye kituo chetu cha afya cha wilaya, ambapo baadhi ya majengo yamekamilika. Kuna majengo saba, hivyo tumeona tuanze kutoa huduma badala ya kusubiri hadi majengo yote kukamilika na hii ni hatua nzuri na tunaishukuru serikali kwa kutupatia fedha hizi,” alisema.

Ntemo alisema mbali ya serikali kutoa kiasi hicho cha fedha, pia imekipatia kituo hicho kipya cha afya madaktari sita, pamoja na wahudumu wengine kwa ajili ya kutoa huduma.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Butamo Ndalahwa, alisema ujenzi huo ulianza Januari, 2019, kwa majengo saba ambayo ni jengo la wazazi, utawala, mionzi, kufulia, dawa, maabara na la wagonjwa wa nje (OPD), huku malengo yakiwa ni kujenga majengo 22 kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari 42.

Alisema ujenzi wa majengo hayo umefikia hatua za mwisho na umeme tayari umeshawekwa katika baadhi ya majengo, huku maandalizi ya kuwekea kwenye majengo mengine yakiendelea.

Alisema hadi kufikia Juni 22, mwaka huu, Sh bilioni 1.6 sawa na asilimia 93 ya fedha za mradi zimetumika kulipia vifaa vya ujenzi na malipo ya mafundi kwa kazi zilizofanyika.

“Kiasi cha Sh milioni 133 sawa na asilimia saba ya fedha za mradi zimebaki kwa ajili ya kuendeleza ujenzi uliobaki pamoja na malipo ya mafundi na matarajio hatua hii itaka milika ndani ya mwezi huu,” alisema.

Ndalahwa alitaja majengo yaliyozinduliwa kuwa ni la wagonjwa wa nje, dawa maabara na mengine yatafunguliwa kulingana na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

Naye Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Christopher Ngendello, alisema changamoto iliyopo ni uhaba wa vifaa tiba na makazi ya watumishi, hali ambayo itazuia utoaji huduma nyakati za usiku.

Alisema changamoto ya usafiri ni kubwa kutokana na barabara kuwa ya vumbi, ambapo kutoka mji wa Mlandizi hadi kwenye kituo hicho ni kilometa saba na usafiri unaotumika ni wa pikipiki.

Alisema changamoto nyingine ni maji, kutokana na laini ya maji kwenda kituoni inatumiwa na watu wengi hivyo maji kuwa machache

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi