loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Balozi Iddi aaga jimboni kwa ahadi

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (pichani), amewaahidi wapigakura na wananchi wa Jimbo la Mahonda, mkoa wa Kaskazini, kwamba ataendelea kushirikiana nao kwa ajili ya kuleta maendeleo hata akiwa nje ya uongozi wa jimbo hilo.

Balozi Iddi alitoa ahadi hiyo wakati akiwaaga wananchi wa jimbo hilo ambalo kwa muda wa miaka 10 alikuwa mwakilishi wake. Alisema kwa muda wa miaka 10 amefanya kazi kwa ajili ya kuleta maendeleo ya sekta mbalimbali katika jimbo hilo, huku kipaumbele kikiwa maji safi na salama, elimu na afya.

Aliwapongeza viongozi wa jimbo la Mahonda kwa ushirikiano wao ambao ulimwezesha kutekeleza kwa mafanikio makubwa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo.

‘’Nawaaga wananchi na wapigakura wa Jimbo la Mahonda kwa utumishi wangu nikiwa Mwakilishi wa jimbo kwani sasa sitagombea tena,’’ alisema.

Katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja, Makame Machano Haji, alimpongeza Balozi Iddi kwa kazi kubwa ya kusimamia maendeleo katika jimbo la Mahonda.

Alisema katika jimbo hilo maendeleo makubwa ya sekta ya elimu yamepatikana, ikiwamo kuwapo kwa madawati na maabara za kutosha katika shule zote za jimbo hilo, hivyo kuondoa tatizo la wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini sakafuni.

‘’Tunakushukuru sana Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda kwa msaada wako katika kuimarisha sekta ya elimu kwa kazi za ujenzi wa madarasa pamoja na usambazaji wa madawati katika shule zote, hivi sasa wanafunzi wote wanasoma wakiwa wamekaa katika madawati,’’ alisema.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitope, Simai Haji, alimpongeza Balozi Iddi kwa juhudi zake kubwa za kusaidia maendeleo katika jimbo hilo, hali iliyopelekea maendeleo ya ufaulu wa wanafunzi.

Alisema idadi ya ufaulu imeongezeka katika shule za jimbo la Mahonda kutokana na juhudi za Mwakilishi za kuweka kambi za matayarisho ya wanafunzi kwa ajili ya kufanya mitihani ya mwisho ya masomo.

Katika sherehe hizo zilizofanyika katika Shule ya Msingi Kitope, Balozi Iddi alikabidhi vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 44 kwa ajili ya tahadhari ya kujikinga na virusi vya corona ikiwamo sabuni, ndoo za maji tiririka na barakoa.

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi