loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kamwelwe amrudisha amrudisha Kaimu Meneja Tanroads

WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isack Kamwelwe (pichani)0 amekiri amefanya kosa kutengua nafasi ya aliyekuwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Pwani, Yudas Msangi.

Juzi akiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya, Waziri Kamwelwe alitangaza kumuondoa Msangi sambamba na aliyekuwa Meneja wa Tanroads Mkoa wa Lindi, Issac Mwanawima kwa kile alichoeleza mameneja hao wameshindwa kusimamia majukumu yao ya kazi, ikiwemo matengenezo na ukarabati wa barabara katika mikoa yao.

Waziri Kamwelwe alisema hayo juzi wakati akifungua mkutano wa 14 wa Baraza la wafanyakazi wa Tanroads uliofanyika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, mkutano uliowashirikisha wajumbe wa baraza hilo kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.

“Nakiri nimefanya kosa kutengua nafasi ya meneja wa Tanroads Mkoa wa Pwani, Yudas Msangi, baada ya kutangaza kutengua nafasi ya meneja huyo na yule wa Lindi nikaona ni vema kujiridhisha, jana (juzi) nimepita katika barabara ile nimeona kazi nzuri aliyoifanya kukarabati barabara katika mkoa wake, nakiri nimemuonea yule mhandisi,” alisema Waziri Kamwelwe.

Hivyo, amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini, Pat rick Mfugale kumrudisha Msangi na kuendelea na majukumu yake ya Meneja wa Tanroads Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na wajumbe wa baraza hilo la wafanyakazi, Waziri Kamwelwe, amewataka mameneja wa Tanroads nchini kutekeleza majukumu yao kikamilifu ikiwemo kuzifanyia matengenezo barabara zote zilizoharibi ka na mvua za masika ili wananchi waweze kuzitumia katika shughuli za maendeleo kwa kuwa serikali imeshatoa fedha nyingi kwa ajili ya kazi hiyo.

Aidha, amewahakikishia wafanyakazi wa Tanroads kuwa Wizara ya Ujenzi itaendelea kushirikiana nao katika majukumu yao ya kiutendaji na kuipongeza Tanroads kwa kazi nzuri inayofanya ya kujenga na kukarabati barabara hapa nchini.

Hata hivyo, alisema licha ya kazi nzuri inayofanywa na Tanroads, changamoto kubwa kwa Tanroads ni muda wa kujenga barabara ambao sio rafiki kwao na kuwashauri kuangalia muda sahihi wa kujenga barabara ambao utawezesha kazi kukamilika kwa wakati.

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Songea

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi