loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bashungwa awapa elimu ya mikopo vijana, wanawake

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa(pichani) ametoa mwito kwa wajasiriamali wanawake pamoja na vijana nchini kutohofia kuomba mikopo kwenye taasisi kubwa za fedha zikiwemo benki, ili kujiepusha na mikopo isiyo rasmi ambayo imekuwa ikiwagharimu kwa kuwatoza riba kubwa na hivyo kuwarudisha nyuma kiuchumi.

Waziri Bashungwa ametoa mwito huo jana wakati akifungua Kongamano la Biashara na Kilimo lililoandaliwa na Jumuiya wa Wafanyabiashara Wanawake na Vijana (TABWA) kwa kushirikiana na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) linalofanyika kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo kwenye uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.

Pamoja na kuipongeza Benki ya NBC kwa mchango wao katika kutoa mikopo ya biashara kwa wanawake na vijana nchini, Waziri Bashungwa aliziomba pia taasisi za fedha nchini kusikiliza vilio vya wanawake na vijana ambao wamekuwa wakilalamikia ugumu wa masharti yanayoambatana na mikopo hiyo ambayo yanakuwa kikwazo kwao.

“Licha ya taifa kuwa na idadi kubwa ya wanawake wenye ujasiri wa kubuni na kuendesha biashara, kasi ya ukuaji wa mitaji yao bado ni finyu, Inafahamika chanzo kikuu cha mitaji yao ni mikopo ya kibiashara ila changamoto inabaki kuwa wengi wao hawana mikopo kutoka kwenye taasisi rasmi za kifedha na matokeo yake wanaangukia kwenye mikopo isiyo rasmi inayowanyonya kwa riba kubwa ndio maana nimeomba benki kubwa ziwasaidie pamoja na kuwaelimisha kama ambavyo Benki ya NBC wanavyofanya, nawapongeza sana,’’alisema.

Kwa upande wake Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya NBC, Jonathan Bitababaje alisema pamoja na kuwajengea uwezo wa kifedha na kiufanisi kwenye biashara, benki hiyo imejipambanua kama kituo kimoja chenye mahitaji yote ya wajasiriamali kwa kutoa huduma mahususi na maalumu zinazoakisi mazingira ya biashara ya ndani kwa lengo la kukuza na kuendeleza wajasiriamali.

“Katika kuhakikisha hilo, benki kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo TABWA na TANTRADE tumeendeleza kliniki kama hizi za biashara pamoja na vilabu vinavyofahamika kama ‘NBC-Club’ ambavyo vinawaunganisha wajasiriamali na kuwawezesha kufanya safari za kibiashara.

Huduma za bure za ushauri wa kibiashara na upendeleo maalumu katika baadhi ya huduma, hatua ambayo inalenga kuwajenga zaidi kibiashara na kiuchumi kwa jumla,”alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TABWA, Doreen Mawala alisema utayari wa wanawake kuomba mikopo unaathiriwa na viwango vikubwa vya riba vinavyotozwa na benki kwa mwaka, dhamana ya mali kuwa ni kikwazo kwa kuwa wengi wao hawana mali kama nyumba au ardhi za kuweka rehani ili wapate mikopo.

Kongamano hilo la siku tatu linahusisha wajasiriamali zaidi ya 400 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Simiyu, Mwanza, Shinyanga na Mara.

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Simiyu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi