loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

…Ndege zaongozana kuleta watalii nchini

ZAIDI ya watalii 177 kutoka mataifa ya Ulaya na Asia, wameendelea kuingia nchini kutembelea vivutio vya utalii. Mashirika ya ndege yamerudisha safari zake na kusema kuwa ujio wao ni matokeo ya kauli ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kuwa nchi ni salama na hakuna virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid- 19.

Akizungumza kwa niaba ya watalii waliowasili 2:15 usiku juzi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), raia wa Ujerumani, Getrude Boldemann alisema kuwa wamefurahishwa na kauli ya Rais Magufuli kwamba Tanzani hakuna Covid -19 ndio sababu wamekuja kutalii. Watalii hao walikuja kwa ndege aina ya Boieng 777 PHBOB ya Shirika la Ndege la Uholanzi (KLM).

Boldemann alisema kuwa Tanzania ni sehemu nzuri, inavutia na kila mtu anatamani kufika kwa kuwa kuna vivutio vingi vya utalii. Awali mashirika ya ndege ya kimataifa na yasiyo yakimataifa, yalisitisha safari kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwapokea watalii hao KIA, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema kuwa kuja kwa watalii hao nchini kumeonesha ushindi dhidi ya ugonjwa wa Covid- 19 Mgwira alisema kuwa kurejea kwa safari hizo, kumeithibitishia dunia kuwa wananchi wa Tanzania wameishinda hofu ya ugonjwa wa Covid-19 na inakaribisha wageni waje kuwekeza na kufanya shughuli za maendeleo.

“Kuja kwa watalii hawa ni ishara ya ushindi mkubwa ni ishara njema ya amani na upendo, hivyo nawaomba wananchi popote walipo watambue kuwa Tanzania ni sehemu salama ya utalii,”alisema Mgwira.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usimamizi na Uwendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KADCO), Christine Mwakatobe alisema kuwa wamejipanga kupokeawatalii zaidi kutoka mataifa mbalimbali kama vile Ujerumani, Uingereza, Ufaransa na wengine wa nchi za bara la Asia.

Mwakatobe alisema kuwa kurejea kwa safari za ndege ya KLM kumetokana na serikali za Uholanzi na Ufaransa ambao ni wamiliki wa ndege hiyo, kuridhika na jitihada za Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid- 19.

“Kuja kwa ndege hii kumetoa matumaini kwa Watanzania na mataifa yote duniani kuwa Tanzania ipo salama, ndio sababu wageni wengi wanaendelea kuja kwa wingi katika mbuga zetu za utalii,”alisema Mwakatobe.

Mwakatobe alisema kuwa Agosti 2 mwaka huu, walipokea ndege ya Shirika la RwandAir 9XR- WL, Juni 01 mwaka huu walipokea ndege ya Shirika la Ethiopia, Julai 30 walipokea ndege ya Shirika la Qatar, Agosti 01 walipokea ndege ya Crystal P4_XTL.

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Moshi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi