loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jeshi la Polisi lajipanga kuzuia uhalifu nchini

JESHI la Polisi limejipanga kusimamia utekelezaji wa sheria ili kuzuia uhalifu na machafuko yanayoweza kutokea katika jamii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi hilo jana jijini Dar es Salaam, utekelezaji wa mradi huo utafanyika kwa lengo la kusimamia utawala na haki za binadamau nchini, ili kutekeleza sheria nchini.

Taarifa hiyo ilisema mradi huo utatekelezwa katika maeneo ya kanda za kipolisi za Zanzibar, Kusini, Mashariki, Ziwa, Kati, Magharibi na Nyanda za Juu Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ambayo hayafuati sheria na kanuni na kukiuka sheria zinazosimamia ujangili kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Kamishna wa Polisi wa Kamisheni ya Ushirikishwaji Jamii, Dk Mussa Mussa, alisema Jeshi la Polisi lipo katika mpango wa mageuzi tangu mwaka 2006 chini ya hati ya mageuzi ya mpango wa marekebisho ya Jeshi la Polisi Tanzania mkakati wa kati wa 2010 /2011 hadi 2014/2015.

"Kazi ya Jeshi la Polisi si tu kusimamia sheria, lakini pia linafanya kazi na jamii kutatua changamoto zinazowaathiri na ndiyo maana kwa sasa tunafanya kazi ya kukagua baadhi ya maagizo ya polisi," alisema.

Alisema programu ya mabadiliko katika Jeshi la Polisi inakusudia kuunda kikosi kitakachotoa huduma kwa jamii katika kuhakikisha linatekeleza jukumu lake la msingi la kulinda usalama wa raia na mali zao.

Dk Mussa pia alishukuru msaada uliotolewa na wadau mbalimbali kama vile Kituo cha Huduma za Sheria (LSF) kwa ajili ya kukuza haki za binadamu na upatikanaji wa haki nchini.

"Jeshi la Polisi linashirikiana na taasisi ambazo tunadhani tunaweza kufanya kazi kwa pamoja na msaada wa LSF unathaminiwa sana na tunatumaini zitaaendelea kufanya kazi na Jeshi la Polisi," alisema.

Alisema jeshi hilo limejipanga kusimamia mfumo wa demokrasia na wa kirafiki zaidi ili kuhakikisha amani na usalama endelevu vinapatikana nchini. Alisema pia madawati ya jinsia na watoto, Polisi-Net na sheria ya uhalifu vitaimarishwa ili kuboresha ufanisi wa shughuli za polisi.

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi