loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watumishi 12 wanaotuhumiwa ‘kutafuna’ mil 307/- kuzitapika

WATUMISHI 12 kati ya 34 wilayani Biharamulo mkoaani Kagera waliokamatwa kwa kupoteza kiasi cha Sh million 307 wamekubali kulipa gharama hizo. Watumishi hao wamesema wameamua kulipa ili kuendelea na kazi huku 12 wakiomba kuongezewa muda wa kulipa fedha hizo na 11 wakiendelea kusalia katika vituo vya polisi wilayani Biharamulo.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jeneral Marco Gaguti alisema wiki hii, watumishi 11 ambao wameshindwa kurejesha hiyo fedha watafunguliwa mashtaka mahakamani.

Hivi karibuni Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) Mkoa wa Kagera kiliomba kutolewa dhamana na kufikisha mahakamani wafanyakazi wa Serikali za Mitaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo waliofikishwa katika kituo cha polisi cha Biharamulo na Lusahunga kwa makosa ya upotevu wa makusanyo ya fedha kiasi cha Sh milioni 307.

Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Kagera, Naseeb Maselle alisema wafanyakazi hao ambao ni watendaji wa vijiji na kata pamoja na wahasibu na watumishi wa vituo mbalimbali vya afya wapatao 34 walituhumiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Juni 23 mwaka huu kwa upotevu wa fedha hizo.

Kupitia kamati hiyo ya chama cha wafanyakazi, ilipata muda wa kujadili malalamiko ya Mashine za Kukusanya Mapato (EFDs) ambazo zimekuwa zikitumiwa na watendaji hao kuwa zimekuwa zikionesha changamoto kadhaaa ikiwemo kutotoa stakabadhi ambayo anapaswa kukaa nayo mkusanya mapato.

“Tunashuhudia mashine wanazotumia polisi, watu wa mistu na mamlaka nyingine kuwa anayetoa listi kwa mteja naye anabaki na stakabadhi, lakini zinazotumiwa na watendaji wetu hazina stakabadhi inayobaki kwa mkusanyaji haya ni mapungufu makubwa,lakini pia wanaokusanya mapato ya halmashauri hawana elimu ya kutosha juu ya kukusanya mapato,”alisema Maselle.

Hata hivyo ,baada ya watumishi hao kukamatwa June 23/mwaka huu, siku tatu baadaye, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Biharamulo, Wende Ng’hala aliamwandikia barua ofisa wa Takukuru Wilaya ya Biharamulo yenye kumb. namba BDC/12/34/vol/11/08 kuwa baadhi ya watumishi walioshitakiwa hawajawai kudaiwa na halmashauri na hawahusi kabisa na upotevu wa fedha, hivyo waachiliwe huru.

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia ...

foto
Mwandishi: Diana Deus, Bukoba

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi