loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtafiti: Kama hutaki kuzeeka kula mtama

ZAO la mtama linaboresha afya ya ngozi, nywele ikiwa ni pamoja na kuweka utimamu katika mfumo wa fahamu ili kuuboresha.

Mtafiti mwandamizi kutoka asasi  ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI), Kituo cha Ilonga kilichopo Kilosa mkoani Morogoro, Ismail Ngolinda alisema hayo kwenye maonesho ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Ngolinda alisema zao hilo pia ni zuri kwa ajili ya lishe ya familia kwa kuwa lina vitamin mbalimbali ikiwemo vitamin B1, Vitamini B2 na BC.

Alisema mtama pia una madini ya magnisiamu kwa wingi nayo yanasaidia kwa ajili ya kuhakikisha  afya ya mifupa ipo vizuri lakini pia afya ya moyo.

Mbali na faida hizo mtama unapunguza mwili usizeeke kwani wale wanaokula mtama uzeekaji wa ogani katika mwili unapungua. 

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi, Bariadi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi