loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Siku zahesabika wagombea ubunge CCM

SIKU zinahesabika ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kabla kufahamika wagombea wake wa ubunge, uwakilishi na udiwani huku ikitarajiwa kushuhudia vilio kwa watakaokatwa baada ya kubainika kujihusisha na vitendo vya rushwa. 

Wakati chama kikiendelea na vikao kabla ya kuweka hadharani wagombea, mbivu na mbichi zinategemewa kujulikana mapema kuendana na ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ya uchukuaji fomu za ubunge, udiwani na uwakilishi. 

Kwa mujibu wa NEC, fomu za kuwania ubunge na udiwani zitatolewa  kuanzia Agosti 12 hadi Agosti 25 katika ofisi za wasimamizi wa uchaguzi za halmashauri za wilaya na makao makuu ya kata. 

Akizungumza jana alipotembelea ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Mpwapwa, Makamu wa Rais, Samia Suluhu alisema chama kinaendelea na mchakato kuchambua wagombea waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali. 

“Watakaobainika kuwa walijihusisha na vitendo vya rushwa tutawakata na kuwaengua kwenye mchakato huo," alisema Samia na kushutumu rushwa kwamba imekuwa mwiba katika kufanikisha uchaguzi huru na wa haki kutokana na baadhi ya wagombea kujihusisha na vitendo hivyo  wapigiwe kura. 

Alisisitiza: "Tuwakatae watoa rushwa katika uchaguzi wa mwaka 2020. Tuna sifa kubwa duniani, naomba tusirudi nyuma. Hili ni suala la kila mmoja wetu kuamua na kutekeleza." 

Alisema mgombea aliyetoa rushwa achaguliwe, hatatumia uongozi kuhudumia wananchi bali atatumia dhamana hiyo kurejesha fedha allizotoa kama rushwa wakati wa uchaguzi.

Alipozungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole
alisema chama kitawashikisha adabu wanaotuhumiwa kutoa rushwa. 

Alisema: “Kuna kamati za usalama na maadili ambazo vikao vinaendelea. Kwa hiyo kwetu sisi ni kama mchakato wa kimahakama hivi. Kwa hiyo nisingeweza kusema sasa hivi kwamba tumepokea kiasi gani (wanaotuhumiwa kwa rushwa) lakini nataka nikuhakikishie, watu wote wabaya waliojishughulisha na vitendo vyote ambavyo ni mwiko kwenye chama chetu, narudia tena, tutashikisha watu adabu.”

Ingawa Polepole hakufafanua ni namna gani watashikishwa adabu, hatua zimeanza kuonekana kutokana na Kamati ya Utelekezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UV-CCM) Taifa kuwaengua wagombea wanne wa ubunge viti maalumu. 

Kaimu Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UV-CCM Taifa, Leonard Singo alidokeza juzi jijini Dodoma juzi kuwa jumuiya imechukua uamuzi wa kuchukua washindi wa pili wa kura za maoni waliokidhi vigezo kwenye mikoa minne ya wagombea hao. 

Katika mchakato wa mwaka 2015, baadhi ya wagombea walioongoza kwa kura nyingi kwenye kura za maoni walitupwa nje na kuchukuliwa mshindi wa tatu huku baadhi ya majimbo yalilazimika kurudia kupiga kura za maoni. 

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi