loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ushindi wampa jeuri Guardiola

USHINDI muhimu wa Manchester City dhidi ya Real Madrid ulioiwezesha timu hiyo kusonga mbele katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya umeanza kumpa jeuri kocha wake, Pep Guardiola.

Guardiola anasema kuwa timu yake imepiga hatua moja mbele kwa mara ya kwanza katika mbio zao za kusaka taji hilo la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Man City wameifungisha virago Real Madrid wanaoshikilia rekodi ya kutwaa mara 13 taji hilo la Ulaya baada ya kuifunga jumla ya mabo 4-2 na kutinga hatua ya robo fainali.

Hata hivyo, Guardiola alisema hakuna muda kwa timu yake kurudi nyuma na kuangalia tena ushindi huo.

"Tuko hapa kwa ajili ya kujaribu na kushinda taji la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, “aliongeza mshindi huyo mara mbili wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya akiwa na Barcelona.

Baada ya ushindi huo dhidi ya mabingwa wa kihistoria Real Madrid, Man City sasa itakumbana na timu ya Ufaransa ya Lyon, ambayo wenyewe waliifungisha virago Juventus ya Italia licha ya juzi kufungwa 2-1.

Lyon imefuzu hatua ya robo fainali kutokana na sheria ya bao la ugenini na sasa itacheza robo fainali, ambayo itaamliwa kwa mchezo mmoja utakaofanyika Lisbon, Ureno Agosti 15.

Mechi zingine zote zilizobaki za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya zitachezwa Ureno, huku nusu fainali ikitegemewa kupigwa kati ya Agosti 18-19 na fainali itafanyika Agosti 23.

"Ikiwa tutafikiria kuwa [kuifunga Real] kunatosha, basi tutakuwa tunajidanganya kwani kama unataka kushinda, basi unatakiwa kuzifunga klabu kubwa, alisema Guardiola.

"Tayari nimezungumza na idara ya utafiti ili kuifuatilia Lyon na wameniambia watanitaarifu. Wachezaji watakwenda Ureno kujaribu kusonga mbele.

MIKEL Arteta amesema hakuumizwa na kipigo cha Arsenal timu yake ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi