loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majaliwa: Sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi inaimarisha viwanda

SERIKALI imeahidi kuendeleza sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi nchini ili kuimarisha uchumi wa viwanda nchini.

Aidha taasisi za fedha na benki nchini pamoja na kutoa mchango kwenye sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi imeelezwa kwamba bado kiasi cha fedha za mikopo knachotolewa ni kidogo mno ukilinganisha na mchango wa hiyo sekta.

Msimamo huo ulitolewa jana wakati wa kuhitimisha sherehe za Nanenane ambazo kitaifa zilifanyika mkoani Simiyu ambako pamoja na masuala mengine, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliwahimiza wakulima kujikita katika kilimo chenye tija.

Majaliwa alisema: “Taasisi za benki kwa jumla zimechangia Sh trilioni 19 kama fedha za mikopo lakini katika fedha hizo sekta ya kilimo imepata Sh trilioni 1.7 tu, hii hairidhishi ni ndogo mno, angalieni na muongeze”.

Majaliwa alisema maonesho hayo yamefana na kusema hakika mchango wa sekta hiyo umechangia kwa kiasi kikubwa pato la nchi na kukua kwauchumi. Alisema kwa miaka mitano sasa, nchi imekuwa na akiba ya kutosha ya chakula na kwamba hayo ni matokeo bora ya kuiwezesha sekta hiyo.

“Mchango wa sekta ya kilimo ni mkubwa kwa maendeleo na ustawi wa nchi, tuna akiba ya kutosha ya chakula, hadi sasa tuna akiba tani milioni 2.79 na maghala yetu yote yana chakula,nchi imejitosheleza,”alisema Waziri Majaliwa.

Akizungumzia jinsi serikali ilivyojizatiti kuboresha sekta hiyo alisema mikakati ilishaanza ambayo ni pamoja na kufuta kodi na tozo mbalimbali kwenye kilimo na pembejeo.

Alisema kwenye upatikanaji wa mbegu bora za kilimo, serikali na taasisi mbalimbali za kilimo nchini imeboresha hali ya upatikanaji wa mbegu ambapo sasa umefikia tani 76,577 na baadhi ya hizo zinazalishwa hapa nchini .

Majaliwa alisema kwenye upatikanaji wa mbolea serikali imehakikisha mkulima anatumia mbolea bora na kwa sasa tani 633,197 za mbolea zipo nchini wakati mahitaji ni tani 576,604.Akizungumzia sekya ya mifugo, Majaliwa alisema nayo inachangia ongezeko kwenye pato la taifa na kwamba serikali inaendelea kuboresha kwa kuhakikisha wafugaji wanafuga kisasa na kupata dawa za mifugo na elimu kwa wakati.

Alisema hivi sasa serikali inaandaa muongozo wa kudhibiti mifugo ili kila mfugaji awezeshwe awe anaogesha mifugo yake huku pia serikali ikiamua kugawa Pori la Misenyi kwa wafugaji ili wakae huko na kupata eneo la malisho lengo ni kuondoa migogoro na wakulima.

Aidha alisema serikali inaendelea kuhakikisha wafugaji wanafuga ng’ombe bora walioboreshwa ambapo hivi sasa ng’ombe wao wanahimilishwa na kupata ndama bora.

Kwenye uvuvi, Waziri Majaliwa alisema serikali inaendelea kuwaelimisha wavuvi jinsi ya kufuga samaki kwa kutumia vizimba ambavyo vimeonesha matokeo mazuri kwa wafugaji samaki kupata kipato kikubwa.

Aidha alisema fursa za uvuvi zimeongezeka katika ukanda wa bahari kuu ambapo vibali na leseni za kuvua eneo hilo na ukanda maalam zinaendelea kutolewa lengo ni kuhakikisha wavuvi na wadau wananufaika na mazao ya uvuvi.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akizungumzia mikakati ya wizara hiyo kuinua kilimo alisema wakulima wameweza kuzalisha tani za chakula milioni 17.5 huku uzalishaji wa mbogamboga ukiongezeka kutoka tani milioni tano hadi kufika tani milioni sita.

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia ...

foto
Mwandishi: Ikunda Eric, Bariadi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi