loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Marufuku vidonge vya folisiki asidi shuleni

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amepiga marufuku utoaji wa vidonge vya asidi ya foliki kwa wanafunzi au wasichana balehe isipokuwa viendelee kutolewa kwa wanawake wajawazito na walio katika umri wa kuzaa.

Alisema pia atamwandikia barua Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako kutoa pendekezo kuanzia Septemba Mosi mwaka huu, kila shule ya msingi na sekondari iwe na kibanda cha maziwa kwa ajili ya wanafunzi kupata lishe ya maziwa.

Akizundua wa Siku ya Lishe na Maadhimisho ya Lishe Kitaifa jijini hapa, Waziri Ummy alisema ni marufuku kuwapa vidonge vya asidi ya foliki wanafunzi na wasichana balehe badala yake fedha zinazotolewa ili kununua vidonge hivyo, zitumike kuanzisha bustani shuleni ili kuzalisha vyakula vinavyotoa madini hayo.

Waziri Ummy alisema fedha ambazo zinatolewa na wadau wa maendeleo kwa ajili ya kununua vidonge vya asidi ya foliki zitumike kuanzisha bustani shuleni kwa ajili ya kuzalisha maboga na matunda mengine ambayo yanazalisha asidi hiyo.

Alisema fedha hizo pia zinaweza kupelekwa kwa vijana ili waanzishe miradi ya bustani za mboga kwa ajili ya kuzalisha mazao yanayozalisha asidi hiyo yakiwemo maboga, matunda na hata karoti badala ya kutoa vidonge kwa wanafunzi.

Kuhusu unywaji wa maziwa shuleni, Waziri Ummy alisema atamwandikia barua Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako ili kutoa pendekezo ili kuanzia Septemba mosi mwaka huu kila shule iwe na kibanda cha maziwa.

Alisema hajapiga marufuku uuzaji wa vyakula vingine shuleni, lakini ataomba katika kila shule hasa za bweni ziwe lazima ziwe na kibanda kimoja cha maziwa na kutumia fedha wanazopewa na wazazi kununua maziwa shuleni na kupata lishe bora.

Kuhusu udumavu wa watoto chini ya miaka mitano ijapokuwa umepungua kutoka asilimia 34.4 mwaka 2014 hadi asilimia 31.8 mwaka juzi, Waziri Ummy alisema bado kasi hiyo haitoshi inatakiwa kufanyika zaidi.

Pia aliomba kuongeza kasi katika kupunguza changamoto ya wanawake kuongezeka uzito na viribatumbo kwa walio katika umri wa kuanza kuzaa kutoka asilimia 29.7 mwaka 2014 hadi asilimia 31.7 mwaka 2018.

Akizungumza Naibu Katibu Mkuu Tamisemi (Afya) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Dk Doroth Gwajima alisema fedha ambazo zinatengwa Sh 1,000 kwa kila halmashauri kwa ajili ya kuimarisha lishe ya watoto zimekuwa zikiongezeka.

Dk Gwajima alisema fedha hizo zilianza kutengwa 2017/18 na kuwa zilipatikana Sh bilioni tisa na zikatumika asilimia 30 tu, 2018/19 zilitengwa Sh bilioni 15 zikatumika asilimia 45.

Katika bajeti ya 2019/2020 zilitengwa Sh bilioni 16.7 na zikatumika asilimia 70, kitendo kinachoonesha utekelezaji wa afua za lishe ulizidi kuongezeka, lakini pia 2020/21 fedha zilizotengwa zimepungua hadi Sh bilioni 12 hata hivyo uwekezaji wa ndani kuhusu lishe umeongezeka kutoka Sh bilioni tisa hadi 11.

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi