loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TARI yafunza wakulima kilimo biashara

TAASISI ya Utafi ti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kituo cha Kifyulilo kilichopo mkoani Mbeya, kinatoa mafunzo kwa wakulima ili wapate uelewa wa mbinu za kufuata ili waongeze tija, uhakika wa chakula, kipato na kuchangia ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini.

Meneja wa Kituo cha Kifyulilo, Dk Juliana Mwakasendo alisema hayo wakati wa maonesho ya nanenane ya kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Dk Mwakasendo alisema ni muhimu wakulima wakatambua kuwa kilimo ni biashara kama zilivyo biashara zingine, hivyo wanapaswa kulima kwa lengo la kuongeza faida kwenye biashara yao ya kilimo ili isiwe ni kwa ajili ya kujikimu kwa chakula peke yake.

Alisema ili kufikia huko wanatoa mafunzo hayo ili waweze kutumia mbinu bora za kilimo, kujua gharama za uzalishaji kwa kutunza kumbukumbu kwani itasaidia kujua bei ya kuuzia, kulima zao na aina ya mbegu zinazohitajika sokoni.

Alishauri wakulima kufuata ushauri wa wataalamu ili kuongeza thamani ya mazao na wapate bei nzuri ikiwa ni pamoja na kujiunga kwenye vikundi ili iwe rahisi kupata huduma kutoka taasisi za kifedha.

Meneja huyo alisema msimu wa kuanzia Julai mpaka Desemba mwaka huu, kituo kilipanga kuwafikia wakulima 600 kupitia mafunzo.

“Mafunzo hayo ni kilimo himilivu kwenye uzalishaji wa maharage, mahindi, viazi mviringo na kilimo biashara na uongezaji wa thamani kwenye zao la maharage na viazi mviringo,” alisema.

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi, Bariadi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi