loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

BoT kuendelea kuimarisha huduma za fedha

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Profesa Florens Luoga, amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango imejielekeza katika kuikwamua Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kuweka Sheria ambazo zinahakikisha kuimarika kwa huduma jumuishi za kifedha.

Profesa Luoga aliyasema hayo alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

“Ushiriki wa Idara na Taasisi za Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na mabenki umeongezeka, hii ni jambo zuri kwa kuwa ni Sekta muhimu katika kukuza sekta ya Kilimo, Uvuvi na ufugaji inayochukua watanzania wengi zaidi ya asilimia 70,” alisema.

Aidha alisema kuwa BOT imejiimarisha zaidi kwa kushirikiana na mabenki, kuhakikisha kuwa huduma za kifedha na uwekezaji katika sekta binafsi inapewa kipaumbele.

Profesa Luoga alisema kuwa kuimarika kwa sekta ya fedha kwenye kilimo, mifugo na uvuvi kutaondoa tatizo la uzalishaji wa msimu kwa kuwa viwanda vinavyotegemea malighafi za kilimo vinaweza kusimama muda wowote kama vitakosa malighafi hizo.

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum, Simiyu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi