loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SUA kuanzisha stashahada ya uzalishaji mbegu

KATIKA kuhakikisha matokeo ya tafi ti na teknolojia mpya za pembejeo zinawafi kia wakulima kwa wakati, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),katika mwaka mpya wa masomo wa 2020/21 kinaanzisha stashahada mpya ya uzalishaji mbegu itakayotolewa maalumu; kwa maafi sa ugani ili nao waweze kusambaza kwa wakulima.

Akizungumzia mkakati wa kuhakikisha matokeo ya tafiti za pembejeo zinawafikia wakulima, Naibu Makamu Mkuu wa Utawala wa SUA, Profesa Maulid Mwatawala alisema chuo hicho kina mkakati wa kufikisha matokeo ya tafiti zote za wakulima ili kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo.

Profesa Mwatawala alisema hayo kwenye maonesho ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu,ambapo awali wakati akifungua maonesho hayo Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan alizitaka taasisi mbalimbali za kilimo nchini kuja na mbinu bora za kutatua changamoto za wakulima ikiwemo matumizi ya pembejeo na jinsi ya kutumia teknolojia mpya za kuboresha kilimo.

Alisema kuanzishwa kwa kozi hiyo maalumu ni hatua mojawapo ya kuongeza uwezo wa maafisa ugani katika masuala ya matumizi ya mbegu bora ili nao wakawasaidie wakulima kuleta tija kwenye sekta ya kilimo.

“Stashahada hii itawawezesha Maofisa Ugani kusambaza matokeo ya tafiti mbalimbali kwa wakulima na kuwaelekeza jinsi ya kuboresha na kulima kwa tija,” alisema Profesa Mwatawala.

Mbali na kuanzishwa kwa kozi hiyo chuo hicho kimeendelea kutoa mafunzo mbalimbali kuhusu mbegu kwa maofisa ugani na wakulima kutoka halmashauri na taasisi mbalimbali nchini.

“Mpaka sasa halmashauri na asasi au taasisi binafsi zinawaleta maofisa ugani ama wakulima kwa ajili ya mafunzo malimbali juu ya ubebeshaji miche ya matunda na jinsi ya kusimamia kitalu cha miche na Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) imekuwa ikiandaa mafunzo mbalimbali kutokana na uhitaji,”alisema Profesa Mwatawala.

foto
Mwandishi: Ikunda Erick, Bariadi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi