loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Juve wamtupia virago Sarri

VIGOGO wa Italia, Juventus wamemtupia virago kocha wao, Maurizio Sarri baada ya msimu mmoja wa kuitumikia timu hiyo.

Sarri aliongoza Juventus kutwaa taji la tisa mfululizo la Ligi Kuu ya Italia, Serie A, lakini timu hiyo imejikuta ikitupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na Lyon katika hatua ya 16 bora. Juve ilishinda 2-1 mjini Turin Ijumaa, lakini timu hiyo ya Ufaransa imesonga mbele kwa bao la ugenini.

Mtaliano Sarri, 61, alipewa mkataba wa miaka mitatu katika kipindi kilichopita cha majira ya joto baada ya mwaka mmoja wa kuifundisha Chelsea katika Ligi Kuu ya England.

Awali, kabla ya kutupiwa virago, Sarri alisema alijitetea baada ya timu yake kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya katika hatua hiyo ya 16 bora.

Timu hiyo ilitakiwa kupindua matokeo ya kufungwa 1-0 katika mchezo wa kwanza kabla ya kuibuka kwa mlipuko wa janga la virusi vya corona huko Ufaransa, Juve ilifanikiwa kushinda nyumbani 2-1 juzi, lakini ilijikuta ikitolewa kwa sheria ya bao la ugenini.

Tetesi zilizagaa kuwa nafasi ya Sarri kwa Kibibi Kizee hicho cha Turin iko katika hatihati licha ya mwezi uliopita timu hiyo kutetea taji lake la Serie A, ikiwa pointi moja juu ya Inter Milan.

MIKEL Arteta amesema hakuumizwa na kipigo cha Arsenal timu yake ...

foto
Mwandishi: TURIN, Italia

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi