loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanaume, acheni kugombea titi na watoto

MILA na desturi zimeelezwa kuwa chanzo cha watoto kupata udumavu nchini.

Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto, Sizaria Andrew kutoka Manispaa ya Iringa anasema ushiriki wa kina baba katika makuzi ya mtoto ni mdogo, na sababu kubwa ni mila na desturi ambapo mama ananyonyesha ziwa moja, lingine ni la baba, kwa madai mila na desturi zinazowazunguka.

Mratibu huyo anasema tabia hiyo, ambapo baba na mtoto kila mmoja kutengewa titi lake, imechangia kudhoofika kwa afya ya watoto wengi kutokana na kukosa kunyonya maziwa ya kutosha.

“Mwisho wa siku mtoto anaingia kwenye udumavu. Mtoto anapozaliwa anatakiwa kupewa ziwa la mama ndani ya saa moja na kuendelea kunyonya miezi sita ya mwanzo hata maji hayaruhusiwi kupewa,” anasema .

Anasema alipowadodosa baadhi ya wanaume walifichua kwamba wao hunyonya matiti ya wake zao ili kuondoa mikosi na kuzuia kuyeyuka kwa ashiki za mapenzi za mama baada ya kuzaa, ambapo baba na mtoto kila mmoja hutengewa titi lake.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali, Mkoa wa Njombe unaongoza kwa kuwa na asilimia 53.6 ya udumavu kutokana na ukosefu wa lishe bora kwa jamii hususani watoto licha ya kuwepo kwa chakula cha kutosha mkoani humo, huku takwimu za kitaifa zinaonyesha asilimia 31 y a watoto chini ya umri wa miaka mitano wana udumavu.

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi