loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakulima Ruvuma washauriwa kuchangamkia miche ya kahawa

WAKULIMA wa Mkoa wa Ruvuma wametakiwa kuchangamkia fursa ya  miche ya kahawa kwa sababu  maeneo mengi  ya mkoa yanafaa kwa kilimo cha zao hilo ambalo limeinua maisha ya watu wengi kiuchumi.

Wito huo umetolewa na mtaalamu wa kilimo, Victor Akulumuka kutoka Kituo cha Utafiti wa zao la Kahawa(Tacri)cha Ugano wilaya ya Mbinga katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji yaliyofanyika viwanja wa Msamala mjini Songea.

Akulumuka alisema wakulima wanatakiwa kuchangamkia fursa ya kulima zao la kahawa kwa kuwa linaonekana kustawi katika maeneo mengi ndani ya mkoa na kilimo ambacho kitainua uchumumi wao na taifa.

Aliwataka wakulima kuzingatia amri kumi za kilimo cha kahawa ambazo zinasaidia katika kustawisha zao la kahawa ambazo zitatoa matokeo chanya na kuongeza uzalishaji wenye tija kwa wakulima .

Alizitaja amri za kilimo bora cha kahawa kuwa ni  kukatia matawi, kutumia mbolea,kupulizia dawa kwa wakati, kupalilia na kuondoa machipukizi. Kupanda miti kwa ajili ya kutunza ubaridi katika shamba.

Aidha alisema endapo wakulima watafuatilia na kusimamia na kufuatilia kilimo cha kahawa mkulima anaweza kuvuna kilo tatu kwa shina moja, ambapo kwa ekari moja mkulima anaweza kuvuna kilo zaidi ya 1,500 kutokana na shamba lenye ukubwa wa ekari moja ambapo hupandwa  miche 540.
 

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Songea

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi